UJENZI KITUO CHA MAFUNZO...BAKANJA



Matukio mbalimbali yaliyojiri katika Ibada ya kubariki kiwanja kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo jipya la kituo cha mafunzo, katika kituo cha walei Taifa cha Isodori Bakanja, Kipawa jijini Dar es salaam. Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Salutaris Libena wa Jimbo Katoliki Ifakara.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi, Richard Sillo, ujenzi huo utagharimu takribani milioni 500, ambapo endapo kila mlei mbatizwa atatoa shilingi mia mbili (200/=) jengo hilo litakamilika na pengine kujenga majengo mengine kituoni hapo. Ametoa wito kwa viongozi wa Halmashauri Walei majimbo na parokia zote nchini kuhamasisha uchangiaji huo wa shilingi mia mbili kwa kila muumini.




Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU