Wakristo waaswa kujinyenyekeza ili kufanikiwa

n Na James Stanley, Arusha.

WITO umetolewa kwa Wakristo wote nchini kuisikiliza sauti ya Mungu na  kulisoma neno lake pamoja na kulitendea kazi  kwenye  maisha yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na kujinyenyekeza mbele za Mungu ili waweze kupokea baraka, amani pamoja na mafanikio.
Wito huo umetolewa na Padri Severien Olesanare Yoshila wa Jimbo Kuu  Arusha katika Parokia ya Mtakatifu.Mathias Ngaramtoni, hivi karibuni katika mahubiri yake kanisani hapo.
“Ni lazima kukubali  kunyenyekea mbele  za Mungu na kuisikiliza sauti yake kila wakati ili kuweza kutembea kwenye ulinzi  wake. Kutosikiliza sauti ya Mungu au kutokuwa  mnyenyekevu  kumekuwa kukileta madhara makubwa kwa  mwanadamu ikiwa ni pamoja na kukosa ulinzi wa Mungu.Pia lazima kutambua sauti ya Mungu inacho tafuta kwa mwanadamu ni  kumfanikisha na kumpa ulinzi utakaomsaidia mwanadamu kutembea kwenye nguvu za Mungu siku zote.” Amesema
Ameongeza  ‘’Watu wengi  wamekuwa  wakishindwa kupokea baraka za Mungu kutokana na wao kushindwa kupata muda wa kulisoma neno na kulitafakari, lazima  mwamini ukubali kufanya kazi kwa bidii na kumpenda Mungu ili uone baraka na mafanikio yadumuyo.”
Padri,Severien amesema Neema ya Mungu humuwezesha mwanadamu kupokea baraka pamoja na mafanikio huku Mungu akiachilia milango ya baraka pale anapopataka.

Aidha amesisitiza ‘’Lazima watu wapambane kwa kufanya kazi kwa bidii na kumpenda Mungu ili waone baraka zake na mafanikio yadumuyo maishani. Na unapotamani   kupata mafanikio lazima utamani kwanza kuongozwa na Mungu, kuwa mnyenyekevu na  kufanya kazi kwa bidii.”

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU