‘Waliopata ujauzito shuleni wabuni njia mpya ya maisha

n Na Emmanuel Kamangu, Kigoma

MKurugenzi wa Utume wa Walei Jimbo Katoliki Kigoma Padri John Mbivilila amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kuliwekea mkazo suala la wanafunzi kutokuendelea kusoma katika shule za Serikali pindi  wanapopata ujauzito wakiwa shuleni.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na gazeti hili ambapo amesema kauli ya Rais Magufuli imekuja kwa wakati muafaka maana Taifa lilikuwa linamomonyoka kimaadili kwa kasi.
“Ukiwaacha waendelee kuzaa halafu warudi shuleni tafsiri yake umeruhusu waendelee kufanya uasherati jambo ambalo ni marufuku  kwani hudumaza maendeleo ya taaluma nchini,” Amesema padri Mbivilila.
Aidha padri Mbivilila amesema kuwa ni kweli wapo wanafunzi hubakwa wakiwa katika umri mdogo ila ni wachache sana ukilinganisha na takwimu ya wanaopata mimba kwa kujitakia, hivyo ni vyema Rais aungwe mkono katika hili ili kupunguza mimba mashuleni.
“Ukimpeleka shule wakati huohuo akiwa na mtoto sasa anaenda kufanya nini kama siyo kupata ujauzito mwingine, kwa kweli lazima kuwepo utaratibu maalumu wakukabiliana na aibu ya namna hiyo kwa Taifa letu,” amesema padri Mbivilila.
Hata hivyo amesema kuwa zamani watoto walikuwa na maadili mazuri kutokana na malezi mazuri ambapo  sasa hivi imekuwa tofauti, mwanafunzi kupata ujauzito imekuwa jambo la kawaida hali ambayo siyo nzuri kimtazamo.
Padri Mbivilila ameongeza kuwa kama mwanafunzi kapendekeza kuzaa basi aendelee na utaratibu huohuo kuliko kurudi shuleni kupata mimba tena na kuwasababishia wazazi gharama zisizo na msingi.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU