WAAJIRI WASIOLIPA MISHAHARA NI MAJIPU-PAPA FRANCIS
Baba Mtakatifu Francisko ameonya waajiri wanaopenda kulipa ujira mdogo wafanyakazi wao kwa makusudi ya kujilimbikizia utajiri , hiyo ni dhuluma , ni kunyonya nguvu wafanyakazi. Matajiri hao ni makupe wanyonya damu na wanatenda dhambi ya mauti. Papa alitoa onyo hilo, wakati wa Ibada ya Misa mapema Alhamisi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta.
Papa alitoa onyo akitafakari somo la kwanza la siku, aya kutoka
Barua ya Mtume Yakobo , ambamo anatoa onyo kali kwa matajiri bahili wanaojilimbikiza mali kwa kunyonya nguvu za wafanyakazi wao. Papa amesema si vibaya kuwa mtu kuwa tajiri , lakini mapato yanayoleta utajiri huo yawe ya haki, na isitokane na kugandamiza wafanyakazi wanaoleta utajiri huo. Papa alieleza na kuhimiza kile kinachoitwa "teolojia ya mafanikio", kwa mujibu wa sheria ya Mungu inayotaka utendaji wa haki , katika kupata utajiri. Papa amesisitiza kwamba, tatizo hasa, ni vigumu kumtumikia Mungu na mali. Ameutaja daima moyo wenye kushikamana na fedha na utajiri , huondoa kirahisi, kiungo katika mnyororo wa uhuru wa kumfuata Yesu. Mtume Yakobo katika waraka wake ameonya waajiri watoa malipo ya haki kwa wafanyakazi wao , kwa kuwa iwapo watawapujwa kilio chao kitafika katika masikio ya Bwana wa haki.
Papa alieleza na kuongeza kukemea kwamba, utajri unazalishwa kwa kuwanyonya wengine , unyonyaji huo husababisha umaskini na hivyo ajir ahiyo inakuw ahaina tofauti na utumwa. Papa alieleza kwa kuzitafakari hali za wafanyakazi wengi leo hii ,ambao wanafanya kazi bila kuwa na mikataba wala bima ya afya baada ya kustaafu. Waajiri kama hao wasiojali hali ya baada ye ya wafanyakazi wao ni wanyonyaji , ni kupe wanaoishi kwa kupata mafanikio kwa nguvu za wenzao wanaowafanyisha kazi katika mazingira yasiyokuwa tofauti na utumwa.
Papa ameuita unyonyaji kazini kuwa ni dhambi ya mauti. Papa alitoa mfano wa watu wanaofanyakazi kwa muda wa saa 11 kila siku na bila mkataba ambao mwisho wa mwezi , hulipwa mshahara Euro 650, na pale wanapodai walau kuongezewa kidogo , hutishwa na mwajiri kama huwataki malipo hayo wa ishie zao, kwani kuna wengine wengi wanaotafuta kazi kama wao. Papa anasema huu ni unyonyaji . Ni kuwafanyisha kazi wengine kama watumwa. Amewatahadharisha matajiri wote wanaofanya dhuruma hizi kwamba , kilio cha damu ya watu hao wanaonyonywa , wanaolilia haki , kinasikika kwa Bwana, kwa kuwa ni kilio kwa haki. Na huu ni utumwa halisi leo hii, ambamo kulidhaniwa hakuna tena watumwa , lakini kumbe wapo wengi tu wanapoishi katika hali ya utumwa , unaofanywa na watu dhalimu mbalimbali kupitia mifumo mbalimbali na hasa wafanya biashara wenye kuwachukua watu wanyonge na maskini , na kuwapeleka katika nchi za nje hasa katiak mataifa ya mbali , Ulaya , Marekani na kwingineko , hasa toka Afrika, na kuwauza huko, ambako huwafanyisha kazi hata zilizo nje ya ubinadamu.
Papa ameeleza na kukumbusha jinisi maisha yanavyoweza kubadilika akitolea mfano wa Lazaro na Tajiri. Jinsi mtu maskini Lazaro alivyopata kibali mbele ya macho yaìMungu na mtu tajiri maisha yake yalivyoingia katika dhiki kubw abaada ya kifo . Papa ametoa wito kwa kila mmoja kutambua hilo kwamba linaweza tokea kwa yoyote anayefanya udhalimu wa kugandamiza wengine. Papa anasema mifano inayotolewa si michezo ya kuigiza lakini ni hali halisi. Na hivyo amemwomba Bwana , atuwezeshe kuuelewa unyenyekevu wa kujali mahitaji ya wengine ambayo Yesu anatueleza katika Injili . Heri kuwa na kidogo kilichopatikana kihalali kuliko utajiri wa mali nyingi iliyopatikana kwa njia ya kunyonya wengine .
Comments
Post a Comment