CANAA YATOA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA MTANDAONI

Mafunzo juu ya uandishi wa habari kwa njia ya mtandao juu ya shughuli za kanisa barani Afrika yameanza jijini Nairobi washiriki wakiwa ni kutoka katika mataifa 10 barani humo ambao ni wanahabari na wasomi katika fani ya uanahabari.
Wawezeshaji wanne watatoa elimu ya uandishi wa habari na uhariri kwa washiriki 30 wanaotarajiwa kuiva vyema katika uandishi wa habari kwa njia ya mtandao.
Baadhi ya mada zinazotolewa ni sifa za habari,muundo wa habari,uundaji wa habari,maudhui ya habari kwa njia ya mtandao,uwasilishaji wa habari za Afrika katika mtandao,hadhira ya kimataifa,mbinu za kufanya mahojiano,matumizi ya sauti na picha,kuandika leads,nukuu pia miiko ya uandishi wa habari za mtandaoni.
Wafadhili wa mafunzo haya ni World Catholic Association for Communications, SIGNIS,na kuandaliwa na Shirika la Catholic News Agency for Africa (CANAA),mradi wa Mababa Askofu wa Afrika chini ya Symposium of Episcopal Conferences of Africa and Madagascar (SECAM).
Baadhi ya mataifa yanayoshiriki ni Nigeria, Ghana, Malawi, Zambia, Tanzania na Uganda.
Mafunzo hayo yanafanyika  katika ukumbi wa Don Bosco Youth Educational Services (DBYES) huko Karen, Nairobi, Kenya.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI