PAPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA MAASKOFU ITALIA



Papa Francis amefungua mkutano mkuu wa 69 wa Baraza la Maaskofu wa Italia CEI Jumatatu hii katika ukumbi wa Sinodi Vatican.
Ajenda kuu ya mkutano huu mkuu wa 69 ni maboresho ya viongozi wa dini katika mabadiliko yanayoendelea.
Katika hotuba yake ya ufunguzi kwa washiriki wa mkutano huo,Baba Mtakatifu amewatia moyo Maaskofu wa Italia kuwasikiliza makuhani wao na kujifunza kutoka kwao.”Jioni hii sitarajii kuwapatia mfumo sahihi wa taswira na umbo la kuhani,lakini hebu wote turejee katika mtazamo wake na kujiweka tayari kusikiliza.Hebu tufikie nyayo zao-mmoja kati ya makuhani wengi parokiani wanaotumia muda katika jamii zetu,hebu tujiulize kwa urahisi,nini hutoa ladha ya maisha?kwa nani na kwanini anafanya huduma hii ya kujitolea?Amesema Papa.
Majibu ya Papa yamehusisha pia kuhimiza urafiki wa kweli na Mungu,kufufua kazi ya uongozi wa kishujaa wa kuhani hasa viongozi wa dini majimboni ambao wamehimizwa kufanya kazi za kimisionari katika kanisa zima ambayo pia ni lazima pia kuwa jukumu la kila maisha ya kikristu na hatimaye ufalme wa Mungu kama lengo la jumla la kanisa na kila mtu aitwaye kutumikia ukuhani.
Mada nyingine za Maaskofu katika ajenda ni pamoja na marekebisho ya hivi karibuni ya sheria juu ya mahakama ya kikanisa pamoja suala la usimamizi wa rasilimali za kiuchumi na mambo ya kisheria na uongozi wa biashara.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU