"MSIANDIKE MABAYA YA AFRIKA TU"
Waandishi wa habari waafrika wametakiwa kutoa kipaumbele kwa habari za bara la Afrika.
Katika hotuba iliyosomwa
na mratibu wa mawasiliano wa AMECEA Padri Chrisantus Ndaga kwa niaba ya
Mwenyekiti wa Catholic News Agency For Africa (CANAA)Askofu Mkuu Charles Palmer
Buckle wa Jimbo kuu Accra Ghana katika mafunzo ya uandishi wa habari za mtandaoni
unaofanyika jijini Nairobi,imeonekana kuwa baadhi ya vyombo vya habari
vinajikita zaidi katika mabaya ya bara la Afrika wakati yapo mambo mengi na
mazuri yanayofanywa na kanisa barani humo hayaandikwi wala kutangazwa.
Mambo yanayopewa kipaumbele
ni pamoja na migogoro,rushwa,magonjwa pamoja na mambo mengine yanayolipa sifa
mbaya bara hilo.
Padri Ndaga ameonyesha
matumaini kwa waandishi wakatoliki waliotoka katika nchi za Kenya, Uganda,
Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Shelisheli, Malawi, Nigeria, Ghana na Sudani Kusini
kuwa watayatumia mafunzo hayo kubadili uandishi unaolififisha bara la Afrika.
Mafunzo hayo ya siku
nne yameandaliwa na CANAA.
Comments
Post a Comment