PAPA APOKEA TUZO YA KIMATAIFA
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa hii majira ya adhuhuri, alipokea Tuzo ya Kimataifa ya Charlemagne kutoka kwa ujumbe wa Bunge la Ulaya wakiwa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Baraza la Ulaya Donald pembe, Martin Schultz na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker.Tuzo hiyo imetolewa kwa Papa kama kutambua juhudi zake katika kutetea Umoja na haki barani Ulaya.
Katika hotuba yake, Papa Francis amesisitiza iwapo Ulaya inapenda kuendeleza heshima na mustakabali wa amani, kwa siku za baadaye katika jamii ya Ulaya , inawezekana tu kuwa hivyo, kwa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu, wenye kuwajumuisha wote.
Na kwamba, kwa ajili ya kuleta moyo mpya kwa ulaya inayoonekana kuchoka, ingawa bado ina nguvu nyingi na uwezekano, Kanisa linaweza na lazima lifanye sehemu yake. Papa Francisko ametaja moja ya utume wake Kanisa ni kutangaza Injili , ambayo leo hii kuliko hata ilivyokuwa siku za nyuma,ni kuhimiza maisha ya kutoka na kwenda kufunga majeraha ya binadamu aliyejeruhiwa, kwa nguvu nyepesi ya kusadiki uwepo wa Yesu, na huruma yake kwamba huleta faraja kwa mioyo iliyopondeka.
Baba Mtakatifu Francisko majira ya saa sita mchana, alipokea kundi la uwakilishi toka Bunge la Ulaya, waliofika Vatican kwa lengo la kumkabidhii tuzo ya mwaka huu ya Bunge la Ulaya ambayo hutolewa kwa mtu aliyeonyesha juhudi zaidi katika kutetea haki na umoja barani Ulaya. Kwa mwaka huu, Tume inayohusika na kuchagua mshindi wa Tuzo , ilimchagua Papa Franciko, kuwa ndiye ameng’ara zaidi katika kutetea haki na umoja wa Ulaya. ,
Hotuba ya Papa , iliendelea kuhimiza Umoja wa Ulaya uendelee kuwa fikra za ubunifu katika uwezo wa kuanza upya katika kufanya mabadiliko chanya katika nafsi ya watu wa Ulaya. Na aliitazama historia ya Ulaya ambayo inaonyesha kwamba, karne iliyopita, Ulaya aliweza kuthibitisha kwamba daima inawezeakana kuwa na mwanzo mpya katika kujenga ubinadamu wenye kuzingatia mazuri, baada ya miaka ya migogoro ya kutisha, iliyofikia katika upeo wa vita ya kutisha, lakini kwa neema ya Mungu, waliweza kuanza tena upya kabisa katika historia ya binadamu. Na kwamba vifusi na majivu ya magofu hakuweza kuzima moto wa matumaini ya wakereketwa waanzilishi wa jitihada za kuanzisha tena na umoja na mshikamano wa watu wa Ulaya. . Wao waliweza kuweka misingi ya ngome ya amani, katika kujenga umoja wa mataifa, umoja si kwa manufaa yao binafsi lakini kwa dhamira ya manufaa ya wote. Ulaya, iliyokuwa imegawanyika kwa muda mrefu , hatimaye ikafuta hali hiyo na kuanza kujenga nyumba yake mpya katika umoja. .
Hotuba ya Papa ilieleza na kutoa mifano mingi ya kihistoria kama ilivyonukuliwa na waandishi na wadhamini wa kidini mbalimbali hatimae akasema kumbukumbu hizi na ziwawezeshe kwa wakati huu , kuleta msukumo mpya katika kukabiliana kwa ujasiri na mfumo wa uharibifu ulioenea katika siku hizi zetu wenyewe. Ni lazima kuwa na hatua za kujituma na kutoa changamoto katika kuleta upya na kuimarisha zaidi na zaidi Umoja wa Ulaya. Papa ameonyesha tumaini lake kubwa kwamba, Ulaya ina uwezo wa kufungua utu mpya unaotokana na uwezo wa Ulaya katika mambo matatu: uwezo wa kuunganisha, uwezo katika mazungumzo na uwezo wa kuzalisha. Na kwamba anayo matumaini yote kwamba, Ulaya itaweza kudumisha na kulinda haki za kila mtu, bila kusahau majukumu yake katika kusaidia wahitaji zaidi.
Comments
Post a Comment