Baba Mtakatifu atuma barua kwa Patriaki wa Kanisa la Kikoptuki juu ya Siku ya Urafiki
Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumanne 10 Mei, alifanya kumbukumbu ya kukutana kwa mara ya kwanza kwa Papa Paulo VI, Askofu wa Roma, na Mkuu wa Kanisa la Kikoputiki la Kiotodosi, Papa Shenouda III, tukio lililofanyika miaka 43 iliyopita. Kwa ajili ya kumbukumbu hii iliyoitwa “Siku ya Urafiki kati ya Wakoptiki Waotodosi wa Misri na Wakatoliki wa Roma, Papa Francisko ameandika barua kwa Mtakatifu Sana Tawadros II, Papa wa Upatriaki wa Alexandria wa Mtakatifu Marko.
Katika barua hiyo,, Papa Francisko ameonyesha kufurahia muungano wa kina wa kiroho kati ya Wakatoliki na Wakoptiki Waotodosi , akimshukuru Mungu kwa hatua za pamoja mpaka sasa kwenye njia hii ya maridhiano na urafiki. Amesema kuwa , ingawa bado ni safari ndefu kufikia muungano kamili wa kukusanyika wote katika meza moja ya Bwana, yaani Ekaristi, kuna hatua za kuonekana zilizopigwa zenye kuwaunganisha mpaka sasa.
Barua hiyo ya Papa Francisko inatoa mwaliko kwa Wakatoliki na Wakoptiki , kutoa jibu la ukarimu katika ujenzi wa moja kamili uliojengwa juu ya msingi wa Injili ya Kristo , na katika kupambana na changamoto za nyakati hizi, hasa Mashariki ya Kati, ambapo Wakristo wanaendelea kukabiliwa na mateso ya kila siku. Kwa ajili yao, amemwomba Mungu Baba Mwenyezi , awajalie faraja za matumaini katika Kristo wale wote wanaopita katika mateso haya, na pia jumuiya ya kimataifa ivuviwe jibu lenye busara na hekima, katika kukiabiliana na uovu huu. .
Baba Mtakatifu ameonyesha hamu yake kwamba, katika wakati huu, wanapoendelea na hija ya maisha hapa duniani ,waweze kujifunza kuvumiliana mmoja kwa mwingine na kubadilishana urithi wa utajiri wa mila za mapokeo , na hivyo waweze kuona wazi kwamba, kile kinacho waunganisha ni kikubwa kuliko vile vinavyowatenganisha.
Papa ameeleza pia akikumbuka mwaka huu ni wa tatu tangu alipokutana naye kwa mara kwa kwanza na Kiongozi wa Kanisa la Kikoptiki la Misri, mkutano wa udugu uliofanyika hapa Roma May 2013, baada ya ukimya wa miaka mingi katika njia hii ya maridhiano na urafiki .
Comments
Post a Comment