"TEC WAFUNDWA"
WAFANYAKAZI
wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) wamepatiwa semina ya siku moja
iliyolenga kuwajengea uwezo wa kufahamu na kuendana na mpango
mkakati wa TEC katika utendaji wao.
Katika semina hiyo iliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano TEC, wafanyakazi hao wameelezwa juu ya umuhimu wa kuzingatia
tunu msingi za Baraza hilo la maaskofu, ili utendaji wao wa kazi uendane na
mabadiliko yaliyomo katika mpango mkakati huo.
Akizungumza na wafanyakazi hao ndugu Stephen Shayo
ambaye ni mwezeshaji katika semina hiyo ameeleza kuwa kuundwa kwa mpango kazi
huo ni matokeo ya tathmini iliyofanywa na Maaskofu ili kuendana na mahitaji ya
utendaji kazi ya sasa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania Padri Raymond Saba amewahimiza wafanyakazi wa TEC kudumu
katika kufanya kazi kwa bidii bila woga ili kuendana na mabadiliko hayo.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteasante
ReplyDeletehongereni sana nawatakia kazi njema
ReplyDelete