PAPA AZIPA SOMO AC MILAN NA JUVENTUS


Wanamichezo na wanariadha wametakiwa kuwa mashahidi wa  maadili halisi ya michezo na riadha katika viwanja vya mashindano. Na daima  kuishi vipaji vyao katika njia zinazoweza ongeza sifa nzuri katika utendaji wa pamoja na mshikamano wa kibinadamu kupitia uadilifu wa michezo na riadha. Ni wito wa Baba Mtakatifu Francisko, siku ya Ijumaa,  wakati akikutana na Wachezaji wa Mpira, Mameneja na Mafundi wa Timu za Juventus na AC Milan, waliokuwa katika maandalizi ya kuchukuana katika Uwanja wa Olimpiki wa mjini Roma, Jumamosi hii, kwa ajili ya fainali Kombe la Italia. Pamoja nao pia walikuwepo wawakilishi wa Ligi ya Taifa ya Daraja la kwanza.  
Hotuba fupi ya Papa kwa wachezaji hao wa mpira wa miguu , alitaja jinsi michezo na riadha vinavyokuwa na  uwezo wa kuwaunganisha watu na kutoa kwa kila mtu  burudani hasa inapofanyika kwa kuzungatia maadili yake halisi, ukweli,  utulivu na amani.  Papa alisisitiza wajibu hao  kwa kila lika na hasa  vijana, katika kujenga maelewano , ujuzi na maadili kwa ajili ya mafanikio ya timu zao,  kwa mashabiki na jamii kwa ujumla.
 Hivyo hotuba ya Papa , iliweka mkazo zaidi zaidi katika utendaji wa  pamoja ili kufikia mafanikio katika michezo, kama ilivyo pia  katika maisha. Alisema  mafanikio ya timu, kwa kweli, ni matokeo ya fadhila  za binadamu katika maelewano, uaminifu, uwezo wa urafiki ,  mazungumzo na  mshikamano. Na pia  ni  suala la uadilifu wa  kiroho,  uliofumbatwa katika maadili ya  michezo. Kwa kutumia  sifa hizi  za maadili, dunia inaweza hata kushinda utendaji hasi unaongamiza  binadamu na dunia kwa ujumla.  
Mpira wa miguu, aliongeza,  pamoja na mapungufu yake na faida zake,  juu ya yote  dhamiri yake  ya ndani, huwa na tumaini linaolomulikiwa na mwanga wa uhusiano na Mungu. Papa alionyesha matumaini yake kwamba, watu wote  hufarijiwa na uwepo wa michezo yenye ladha ya udugu, maelewano, kuheshimiana na hata kusameheana.  Aliwataka wachezaji , kabla ya kuwa mabigwa wa michezo, lakini kwanza wawe mabingwa wa maisha adilifu.  Na kwamba kuinuka katika michezo daima ni jambo jema na vizuri inapokuwa  ushuhuda wa dhati kwa maadili ambayo yanapaswa  kuwa  sifa na tabia za kweli  za  michezo. Na hivyo Papa aliwataka wasiwe na wasiwe na hofu ya kujichanganya kwa  utulivu na usawa katika ulimwengu wa kimaadili na kanuni za dini,  yenye kuhamasisha michezo katika maisha matulivu.
Kwa mtazamo huo,  Papa alihitimisha kwa kuwatia nguvu wanamchezo hao , kuufanya michezo wa mpira wa miguu, kuwa nyezo ya kutoa ujumbe  chanya  wa maelewano na mshikamano kwa  jamii nzima.
Baada ya kukutana na Papa , Makocha wawili wa timu hizi mbili , AC Milan na Juventus, Christian Brocchi na Massimo Allegri, walitoa maoni yao , wakisema  kukutana kwao na Papa Francisko ulikuwa ni wakati wa mzuri na wa kusisimua na hasa Papa alipoonyesha kutambua thamani ya mchezo huu wa mpira wa Miguu, kuwa  kati ya viungo bora katika mnyororo wa  maisha matulivu  ya kijamii.  Walisema hotuba ya Papa itaendelea kubaki mioyo mwao kama dira ya maisha yao kama wanamichezo . Imewasaidia sana kuwajenga kifikra kwamba michezo yenye kufuata maadili si dhambi, lakini kipengere muhimu katika kuiunganisha jamii bila ubaguzi. 

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI