KOMESHENI NDOA ZA JINSIA MOJA-RUWA'ICHI
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki Mwanza Yuda Thadei
Ruwaichi amekemea vikali ndoa za jinsia moja na kusema sasa ni wakati muafaka
kwa jamii kuzikomesha.
Amekemea ndoa hizo jijini Mwanzakatika misa takatifu
ya azimisho la sikukuu ya wakina baba iliyofanyika katika parokia ya Kawekamo
jijini humo.
Askofu Ruwaichi amesema hakuna familia yoyote
takatifu inayoweza kutengenezwa na watu wawili wa jinsia moja walioamua kuishi
pamoja kindoa.
Amesema ndoa takatifu ni ile ya mme na mke kuoana na
kupata Baraka zote za Mwenyezi Mungu.
“Watu wanamkosoa Mwenyezi Mungu kwa kuamua kuoana
mme kwa mme ama mke kwa mke na kuamua kuasili watoto kitu ambacho hakikubaliki
katika dini yoyote”Amekemea Askofu Ruwaichi.
Amelaumu tabia za baadhi ya mataifa makubwa
yaliyoendelea kuyashauri mataifa madogo yanayoendelea kukubaliana na tabia hizi
alizoziita”chafu” kwa kisingizio cha misaada na haki za binadamu.
“Mwenyezi Mungu alikuwa na maana kubwa kuweka ndoa
takatifu ,kutoa zawadi,tunu,furaha,upendo na Baraka kwa mke na mme walioamua
kuishi pamoja na kujenga familia,sasa iweje leo mwanadamu apinge hilo?”Amehoji
Amewataka wanafamilia(mke na mme)kuishi kwa
amani,furaha,upendo na imani kwa Mwenyezi Mungu ndani ya familia hasa kwa
kuzingatia kuwa muunganiko huo ni kanisa la nyumbani.
Sambamba na kemeo hilo,Askofu mkuu amewataka mapadri
wote wa Jimbo kuu Mwanza kuitafsiri,kuifundisha na kuisambaza hati
fundishi(furaha ya upendo)katika kila Jumuiya ili iziboreshe familia.
Hati hiyo inatoka kwa Baba Mtakatifu Papa Francisko
lengo lake likiwa kuziimarisha familia takatifu.
Bernard James,Mwanza
Comments
Post a Comment