"TUMEJIPANGA KWA KONGAMANO"-ASKOFU MKUU RUWA'ICHI


Askofu mkuu wa jimbo kuu Mwanza Jude Thadeus Ruwa'ichi ameitaka kamati kuu ya maandalizi ya kongamano la Ekaristi Takatifu litakalofanyika jijini Mwanza June kutekeleza majukumu yake kwa muda muafaka ili kongamano hilo lifanyike kwa mafanikio makubwa

Askofu Ruwa'ichi ameyasema hayo katika mkutano wa kutathmini maendeleo ya maandalizi ya kongamano la Ekaristi Takatifu uliofanyika katika parokia ya Kawekamo na kuhusisha wanakamati pamoja na ugeni kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki TEC.

Amesema kila kamati inatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa kujituma na uhakika zaidi ili kufanikisha tukio hilo la kihistoria.

Amezitaka kamati zote kushirikiana kwa hali na mali katika utendaji wa kila siku mpaka kongamano litakapokwisha.

Ameshauri kamati kuu kuhakikisha inajipanga vizuri ili baada ya kongamano kusibaki madeni yoyote yale na kila kitu kiwe katika hali nzuri.

Kamati kuu pamoja na ugeni kutoka TEC wamefanya ukaguzi wa maandalizi ya kongamano hilo kwa kukagua miundombinu,mkakati wa mawasiliano,mazingira,maandalizi ya watoto,muitikio wa waamini,usafiri n.k huko Bujora,Kawekamo,Nyegezi seminari.

Ugeni kutoka TEC ulioongozwa na Padri Gallus Malandu umeridhika na namna maandalizi ya kongamano yanavyoendelea.

Baadhi ya kamati zilizowasilisha bajeti zao ni pamoja na mawasiliano,utoto mtakatifu,mapokezi/malazi/itifaki,chakula,ulinzi,afya,mapambo,liturujia.

Kongamano la Ekaristi Takatifu kitaifa litafanyika jijini Mwanza katika Parokia ya Kawekamo kuanzia tarehe 8-12 June 2016

Bernard James,Mwanza
                                        









                             














Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI