Wanaokimbilia miujiza ya uponyaji watahadharishwa
WITO umetolewa kwa waamini
nchini kuacha kutafuta uponyaji wa magonjwa yao kwa njia za mkato badala yake
wajiaminishe kwa Mungu na kwenda sehemu sahihi ya kupata huduma za tiba.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza
Mhashamu Yuda Thadei Ruwaichi, katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Siku ya
Wagonjwa duniani, iliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya
Bugando, jijini Mwanza.
Askofu Ruwaichi amewataka baadhi ya waamini wanaokimbilia uponyaji kwa
miujiza kujitafakari na kufanya maamuzi sahihi kwa kuiga mfano wa Kristo ambaye
katika magumu yote aliruhusu mapenzi ya Mungu yatimizwe.
“Nimeona matangazo mengi yanayowaalika watu waende kuponywa kwa miujiza,
na pia huko mnakimbilia wengi. Najua huwa mnaenda wengi. Hebu mjikusanye
vizuri, mtafakari na mfanye lile lililo sahihi” ameeleza Askofu Ruwaichi.
Aidha ametoa wito kwa waganga, wauguzi na wote wanaohusika kuwahudumia
wagonjwa kujenga utayari na moyo wa kusikiliza kwa dhati, kwa kuwa wagonjwa
wengi, hasa wale wanaokimbilia kutafuta majibu pasipo na majibu, wanaenda
mahali wanapoamini wanasikilizwa.
“Siyo kusikiliza kama mtu aliyekereka, bali kusikiliza kama mtu ambaye
anatimiza wito mtakatifu aliojaliwa na Mungu wa kulinda na kusaidia uhai wa
binadamu ustawi na kuendelea” ameongeza.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya Saratani katika Hospitali
ya Rufaa Bugando, Dk. Nestory Masalu ameeleza kuwa kukithiri kwa magonjwa sugu
yasiyo ya kuambukiza kunasababishwa na tabia ya watu wengi kukimbilia tiba
mbadala ambazo husababisha kuacha kutumia dawa walizoshauriwa kutumia.
Akitoa mada katika siku hiyo ya wagonjwa duniani ambayo kitaifa
imefanyika Jimbo kuu Katoliki Mwanza, Dk. Masalu amesema kuwa kutokuwa na
desturi ya kupima afya husababisha mgonjwa kutumia dawa nyingi pale ugonjwa
unapogundulika.
“Kumekuwa na uelewa mdogo wa magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza. Watu
wengi wamekuwa wanatumia gharama kubwa kwa tiba mbadala, wakiwa na imani au
kuaminishwa kwamba watapona, na hivyo kuacha dawa za hospitali. Matokeo yake
hao wagonjwa huja na hali mbaya sana hospitali na wakati mwingine inakuwa ngumu
kutibika” ameeleza.
Aidha katika kukabiliana na magonjwa sugu yasiyoambukizwa uongozi wa
Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa kushirikiana na Idara ya Tiba imeweka mipango
ya muda mrefu ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni pamoja
na kuadhimisha siku za magonjwa husika kama figo, sukari na moyo na shinikizo
la damu, ambapo hufanya uchunguzi wa bure na kutoa ushauri kwa magonjwa husika.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amelishukuru Kanisa Katoliki kwa kutenga fursa ya
kuwakumbuka na kuwaombea wagonjwa, kwani daima limekuwa mdau mkubwa katika
sekta ya afya.
Aidha Mongela ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ametoa
rai kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kufanya mazoezi ili waweze
kuimarisha afya zao na kujikinga na maradhi mbalimbali.
Jimbo Kuu la
Mwanza kuadhimisha siku ya wagonjwa kila mwezi
Katika hatua nyingine Askofu
Ruwaichi ameziagiza parokia zote za Jimbo Kuu Katoliki Mwanza
Comments
Post a Comment