"Mkristo awe mtumwa wa upendo na siyo uwajibu tu" Papa Francisko
Wagumu wanaogopa uhuru tunaopewa na Mungu, wanaogopa upendo.Ni maneno ya baba Mtakatifu Francisko wakati wa misa yake ya asubuhi Jumatatu 6 Februari katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha Mjini Vatican, akisistiza juu ya mkristo kuwa mtumwa wa upendo na siyo tu kuwajibika, anawaalika waamini wasijifiche katika ugumu kwa kushirikia na kujificha nyuma ya amri .
Mahubiri ya Baba Mtakatifu yamegusia Zaburi ya 103 kwenye kiitikio “Bwana wewe ni mkubwa na kwa maajabu yako, na pia somo la kwanza kutoka katika kitabu cha Mwanzo, Anasema Bwana anafanya kazi kwaajili ya kutenda maajabu katika uumbaji na kumfanya mwanae awe wa maajabu ya uumbaji wake mpya.Ametoa mfano kwamba ,siku moja mtoto mmoja aliuliza swali ya kwamba Mungu kabla ya kuumba ulimwengu alikuwa anafanya nini , na yeye alimjibu alikuwa anapenda, na pia kwasababu gani aliumba ulimwengu?.

Kwa jibu rahisi ni kushirikishana ukamilifu wake. Kwa kuumba ulimwengu pia alimtuma mwanae aweze kutengeneza upya.Kwani Mungu anatengeneza kitu kizuri kutoka katika kibaya, anatoa ukweli kutoka katika makosa na kufanya wema kutoka katika ubaya.Akikumbuka mojawapo ya sehemu za Injili Baba Mtakatifu Francisko anasema,Yesu alipo waambia watunga sheria ya kwamba “Baba yangu daima anafanya kazi,wamdhihaki na kuchukia hadi kutaka kumuua, kwaajili ya kauli hiyo, je ni kwanini, ni kwasababu hawakujua kupokea mambo ya Mungu kama zawadi, bali waliona haki hiyo kama vile ni amri.Baba Mtakatifu anasema ni wachache ambao wanafanya kazi zaidi. Badala ya kufungulia mioyo yao kupokea zawadi, wao ni kujificha chini ya ugumu wa amri, na sheria walizokuwa wametunga hadi kufikia 500 au zaidi.Hiyo yote ni kutkana na kwamba hawakujua kupokea ile zawadi, kwa maana ili kupokea zawadi ni lazima kuwa huru, hawa walikuwa ni wagumu na wamejaa hofu ya kuwa na uhuru wa Mungu alio kuwa nawajalia kama zawadi , hivyo walikuwa na hofu ya upendo.
Anaendelea kufafanua kwamba ndiyo maana Injili inasema baada ya Yesu kutamka juu ya kazi ya Baba yake anayotenda walitaka kumuua, kwasabau kasema kwamba Baba anatenda maajabu kama zawadi hii ya kupokea zawadi ya Baba! Ndiyo maana leo hii tuna msifu Baba kwamba, wewe ni mkuu, tunakupenda kwasababu ya zawadi yako, umeniokoa na umeniumba.Hiyo ndiyo sala ya sifa,ya furaha , na ni sala inayoleta furaha ya Mkristo.Hiyo siyo sala iliyofungwa na wala na kwamba ni ya mtu mwenye huzuni ambaye mara nyingi kajifunga mwenyewe hatambui namna ya kupokea zawadi.Baba Mtakatifu anasema huyo ni mtumwa anayewajibika tu na siyo katika upendo wa kweli. Baba Mtakatifu anatoa ushauri kwamba mtu anapogeuka kuwa mtumwa wa upendo, huyo ndiye ni mtu huru,na huo ndiyo utumwa mzuri.Yapo maajabu mawili yaaani kazi ya uumbaji na maajabu ya kukuombolewa kwa maana ya kuumbwa upya, ndiyo tunayopaswa tujiulize je ninaipokea vipi zawadi kutoka kwa Mungu, ya uumbaji?, iwapo ninaipokea kama zawadi , nitapenda kazi ya uumbaji , nitalinda mazingira , na hiyo ndiyo zawadi.
Kwa kumalizia mahubiri yake Baba Mtakatifu anasistiza , ninapokeaje ukombozi na msamaha ambao Mungu amenipatia ili kuweza kuwa kama mwanae wa upendo kwa ukarimu na huru, au nina jifìficha katika ugumu wa amri zilizofungwa , na daima zenye kiza ambazo hazikupatii furaha kwasababu haupati uhuru. Kila mmoja aweze kujiuliza namna ya kuishi na kutekeleza maajabu hayo mawili ya uumbaji na kuumbwa upya.
Mungu aweze kutufanya tutambue haya juu ya kuumbaji wake wa ulimwengu,na kutufanya tutambue upendo wake alio nao kwetu sisi, na baadaye nasi tuweze kutamka kwa kiitikio cha zaburi ya wewe ni mkuu ee Bwana.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
Comments
Post a Comment