Askofu Chengula awataka vijana kujiunga na mashirika ya kimisionari

ASKOFU wa Jimbo Katoliki Mbeya Mhashamu Evarist Chengula (IMC) amewaalika  vijana wa kiume na kike kuguswa na wito wa Shirika la wamisionari Wakonsolatha na kwamba wanafanya kazi yoyote kadri ya mazingira.
Ametoa wito huo kwenye adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya kutolewa Bwana Hekaluni, siku ya watawa  iliyoambatana na adhimisho la miaka 20 ya  Daraja Takatifu la Uaskofu wa Askofu Chengula katika Kanisa kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Anthony wa Padua Parokia ya Mbeya Mjini.
Amesema  Shirika la wakonsolatha linawapokea vijana wa kike na kiume  waliohitimu kidato cha 6 na kwa waliojifunza Theolijia watapelekwa Morogoro kujifunza masuala la falsafa na mafunzo mengine.
“Ni shirika la Kitawa lina misimamo yake  mbalimbali, jambo la kwanza  sisi  tunaitwa  Ekaristia watu wa kuabudu na jambo la pili ni watu wa familia na kufanyakazi leo kama ndiyo mwisho hautafanyakazi tena sehemu nyingine(kujituma) mradi tu ufanye kazi vizuri na muwe tayari kufanya kazi na mtu yeyote, kama ni mbaya basi muite Mungu akurudishe kama ni mzuri basi Mungu anakuangalisha,” amefafanua.
Katika Ibada  hiyo masista, mapadri  na mabruda kutoka mashirika mbalimbali ya Kanisa Katoliki   wamepita  Altareni  kuelezea  utume wao na kuwaalika wazazi kuwaruhusu kujiunga ikiwemo na vijana  kujiunga na miito hiyo mitakatifu.


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI