Mama Janeth Magufuli atoa msaada kwa wazee Tabora
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Awamu ya tano Mama
Janeth Magufuli ametoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa wazee na
walemavu katika kijiji cha Amani Ipuli Tabora na kuwaomba wanatabora kuwa na
moyo wa huruma kwa wazee na wahitaji.
Mama Janeth ametoa unga
wa mahindi kilo 3521, mchele kilo 3125, maharage kilo 1250, mafuta ya kula ,
sabuni za kufulia, mafuta maalumu ya kupaka kwa watoto walemavu wa ngozi na
vitu vingine muhimu kwa wazee wa kituo hicho.
Pia ametoa msaada wa
vitu mbalimbali katika gereza la Mahabusu Tabora maarufu kama gereza la Zuberi.
Naye Katibu Tawala wa
Mkoa wa Tabora Dr. Tea Ntara
amemuhakikishia Mama Janeth kuwa serikali ya mkoa imejipanga vizuri na
hivyo misaada yote itawafikia kwa utaratibu na hakuna kitu kitakachopotea.
Wakati huo huo Mbuge wa
Tabora mjini kupitia viti maalumu (CCM) Mwanne mchemba amemhakikishia Mama
Janeth kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dr.
John Pombe Magufuli dhidi ya vita vya dawa
za kulevya ambazo zinayoharibu vijana na Taifa hili.
Naye Afisa Ustawi wa
Jamii Manispaa Tabora Baraka alitoa baadhi ya changamoto zinazokikumba kituo
hicho cha wazee cha Amani, Ipuli na Tabora kuwa ni ukosefu wa usafiri, uchakafu
wa majengo, vyoo vya kudumu na mabafu, upungufu wa wahudumu, uvamizi wa maeneo
ya kijiji hicho na mavazi kwa wazee wanaoishi mahali hapo.
Mama Janeth Magufuli
alifuatana na Mama Merry Majaliwa mke wa Mh . Waziri Mkuu wote kwa pamoja wakiwahimiza wananchi kuwa na moyo wa ukarimu kwa watu
wenye shida.
Shughuli hiyo ya kutoa
msaada kwa wazee na watu wenyeshida ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya na
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mh Hamis Kigwangala, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa
vyama vya siasa, viongozi wa Dini na
wanainchi wa manispaa ya Tabora.
Kituo hicho kilianzishwa
mwaka 1969 kama kituo cha kulea wazee waliokuwa wametengwa na ndugu zao baada
ya kupata ugonjwa wa ukoma sasa kipo rasmi chini ya Uangalizi wa Manispaa
ukipokea watu wote waliotengwa na jamii zao.
Comments
Post a Comment