Padri akemea watoto kuvalishwa hirizi
WAAMINI wameonywa
kutojihusisha na imani potofu kwa kuwavalisha watoto wao hirizi na vitu
visivyokubalika mbele za Mwenyezi Mungu.
Onyo
hilo limetolewa na Padri Wanyonyi Simiyuss kwenye ibada ya kuwabatiza watoto
iliyofanyika katika Parokia hiyo ambapo amewataka waamini kuachana na tabia
hiyo ya kuwavalisha watoto hirizi.
Amesema
kuwa Mungu mwenyewe hakubaliani na hilo kwa kuwa suala hilo linaashiria kuwa ni
la kishirikina na linakubaliwa na shetani mwenyewe.
Amesema
kuwa kitendo cha kuwavalisha watoto wadogo hirizi na vitu vinginevyo
visivyokubalika mbele za Mungu ni ishara kubwa inayoonyesha kushiriki ibada za
kishirikina za kishetani ambazo hazina nafasi kwa watoto hao ambao ni wadogo.
“Kitendo
hicho cha kuwavalisha hirizi na shanga ambazo hazina maana yoyote mbele za
Mungu, sitokubaliana na jambo hilo na kila nitakapofanya ibada ya kuwabatiza
watoto itabidi nifanye kwanza uchunguzi na kama watabainika sitohusika na
dhambi hiyo.”Amesema.
Hata
hivyo amewataka waamini hao kumtolea Mwenyezi Mungu zabihu iliyonona ili waweze
kubarikiwa ikizingatiwa kuwa ni agizo na lipo kwenye maandiko ya Biblia.
Amesema
haipendezi kuona wakristo haohao wanatoa vitu vyenye thamani kubwa kwenye
sherehe kama vile za ndoa, kicheni pati na kumbukumbu ya kuzaliwa, lakini
linapofikia suala ya kumtolea Mungu hawafanyi kama huko kwingine.
“Harusi,
kicheni pati kumbukumbu ya kuzaliwa vitu hivyo waamini wapo mstari wa mbele
katika kuchangia, lakini suala la kumtolea Mungu zabihu iliyonona ni vigumu
kwao hii kwa kweli inasikitisha tena ni dhambi na mnatakiwa kutubu tu,”amesema.
Padri
huyo pia amewataka wasimamizi wa watoto waliobatizwa kwenye ibada hiyo
kuhakikisha shetani hawatumii katika vitendo viovu, bali kinachotakiwa wawape
malezi bora na misingi ya kiroho itakayowafanya kumpenda Mungu wao.
Amesema jukumu la kuhakikisha watoto hao wanapata
malezi hayo pia lipo kwao kwa kushirikiana na wazazi wao ambapo kwa kufanya
hivyo taifa litaweza kuwapata viongozi ambao watakakuwa wacha Mungu na
waadirifu kwa serikali.
Comments
Post a Comment