BREAKING NEWS: ASKOFU CASTORY MSEMWA WA JIMBO KATOLIKI TUNDURU MASASI AFARIKI DUNIA
Msiba mzito
Na Bernard James, DSM.
JIMBO Katoliki Tunduru Masasi limempoteza Askofu wa
Jimbo hilo Mhashamu Castory Msemwa( katikati pichani) aliyefariki leo majira ya saa 7
mchana nchini Oman.
Kwa mujibu wa Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru
Masasi, Padri Jordan Liviga, Askofu Msemwa amefariki dunia akiwa mjini Muscat
(Oman), akiwa safarini kwenda nchini India kupata matibabu ya maradhi
yaliyokuwa yakimsumbua.
“Amefia nchini Oman wakati akienda kupata matibabu
nchini India. Akiwa nchini humo amezidiwa ghafla na kupoteza fahamu, hadi
umauti ulipomkuta.”
Marehemu Msemwa amekuwa na tatizo la kiafya kwa
kipindi cha miaka miwili, na amekuwa akipata tiba mbalimbali na kuendelea na
utume kama kawaida.
Aliondoka nchini siku ya Jumatano wiki hii kuelekea
nchini India kwa matibabu kabla hajafariki dunia.
Padri Liviga amebainisha kuwa utaratibu wa kuuleta
nchini mwili wa marehemu Askofu Castory Msemwa siku ya Jumapili Dar es Salaam
unafanyika. Taarifa zaidi za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadaye.
Askofu Castory Paul Msemwa amezaliwa mwaka 1955
katika kijiji cha Kitulira, Parokia ya Matola Jimbo Katoliki Njombe. Alipata
elimu ya msingi katika shule ya Motola, kisha Sekondari katika Seminari Kuu ya
Peramiho ambapo alisomea Falsafa na Teolojia kati ya mwaka 1981 na 1987. Alipata
daraja ya Upadri tarehe 7 Juni 1987. Amekuwa Paroko Msaidizi, Kiongozi wa
vijana parokiani jimboni Njombe, mwalimu na amesoma katika Chuo cha Teresianum
Pontifical College for Spirituality huko Roma na kuhitimu mwaka 1996. Alipata
Daraja ya Uaskofu tarehe 30 Januari 2005 kisha kusimikwa kuliongoza Jimbo
Katoliki Tunduru Masasi tarehe 25 Agosti 2005.
Mwenyezi Mungu ampumzishe pema mbinguni, Amina.
Mungu ampe pumziko la milele.
ReplyDeleteAmina.
Raha ya milele umpe EE Bwana Na mwanga wa milele umuangazie astarehe kwa amani. Amina
ReplyDeleteRaha ya milele umpe eeh Bwana apumzike kwa amani amina
ReplyDeleteRaha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie. Amina
ReplyDeleteRaha ya milele umpe eee Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie, apumzike kwa amani. Amina
ReplyDelete