ACHENI UKRISTO LEGELEGE-ASKOFU NZIGILWA
ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es
salaam Mhashamu Euzebius Nzingilwa ,amewakumbusha wakristo
wote kuwa Yesu Kristo havutiwi na ukristo legelege, hivyo kila mtu anapaswa kuwa chumvi
na nuru kwa wengine kwa kuyaishi vyema maisha ya kiimani.
Akizungumza kwenye
mahubili ya ibada ya
misa takatifu ya hija ya Umoja wa
Wanaume Katoliki (UWAKA) kijimbo iliyofanyika Bagamoyo, Askofu Nzigilwa
amesema Bagamoyo ni mahali pa kufukuza
giza na kuonyesha njia
itakayomfanya mkristo ajue wapi akanyage
na wapi asikanyage.
“Ninyi ni chumvi na
nuru ya ulimwengu, itumieni karama
hiyo kuangaza mwanga palipo na giza, kila
mmoja anatakiwa kujiuliza
tangu asubuhi hadi jioni amezuia
maovu kiasi gani au kwanini amekuwa
chanzo cha maovu
na si kukasirika wala kukunja ndita
za uso, bali upole na unyenyekevu uchukue hatamu kwa maana unyenyekevu
haupimwi kwa action bali hupimwa kwa
reaction”.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa UWAKA
Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam
Amedeusi Moshi amemshukuru Askofu,
mapadri na watawa wote kwa ujumla
waliotoka parokia mbalimbali
na kushiriki pamoja
katika hija hiyo huku akiwataka
wanaume katoliki kila parokia kuchangia shilingi
laki tano (5) kwa ajili ya maboresho ya wafia dini kituo cha hija cha Pugu Jjimbo Kuu Katoliki Dar es
salaam.
Kwa upande wake Katibu
wa UWAKA Jimbo na taifa, Julius
Kansonso amesema nia hasa ya hija
ya Bagamoyo ilikuwa ni kuwaombea wanaume
wote ili watambue na kuuishi kwa vitendo wajibu walionao kwa Mungu, kwa umma, kwa Kanisa na
kwa familia.
Comments
Post a Comment