Ujumbe wa Papa Francisko kwa Kipindi cha Kwaresima 2017
Baba Mtakatifu Francisko anasema, maskini wanaolala mlangoni pa matajiri si kero inayopaswa kushughulikiwa kama “chuma chakavu” bali ni mwaliko wa kutubu na kumwongokea Mungu sanjari na kubadili mfumo wa maisha tayari kuwakumbatia na kuwasaidia wengine katika shida na mahangaiko yao. Changamoto kubwa wakati wa Kipindi cha Kwaresima kwa mwaka 2017 ni kujitahidi kumwilisha sehemu ya Injili la Lazaro maskini na tajiri asiyejali wala kuguswa na mahangaiko ya jirani zake. “Neno ni zawadi; jirani yako ni zawadi pia”. Hii ndiyo kauli mbiu inayoongoza ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko katika kipindi cha Kwaresima kwa Mwaka 2017, muda wa kusali, kutafakari, kujikita katika maisha ya Kisakramenti, lakini zaidi kumwilisha matendo ya huruma kiroho na kimwili kama kielelezo cha imani tendaji! Baba Mtakatifu anasema, Kipindi cha Kwaresima ni mwanzo mpya na njia inayowaelekeza waamini katika maadhimisho ya Siku kuu ya Pasaka, kielelezo cha ushindi wa Kristo Yesu dhidi ya dhambi na mauti, muda w...