"MAPADRI WAZINGATIE WITO"



ASKOFU wa Jimbo Katoliki Njombe Mhashamu Alfred Maluma amewakumbusha mapadri nchini kuuzingatia wito wa upadri kwa kutekeleza kwa umakini ahadi walizoweka siku walipopewa Daraja ya Upadri hasa kuzingatia kuwa Bwana Yesu Kristo, ambaye Baba alimpaka mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu, atawalinda kwa ajili ya kuwatakasa wakristo na kumtolea Mungu sadaka.

Ameyasema hayo katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki Njombe wakati Jimbo hilo likifunga rasmi Mwaka wa Jubilei ya Upadri na pia kumshukuru Mungu kwa zawadi ya mapadri wanne (4) waliosherekea Jubilei ya Miaka Ishirini na tano (25) ya Upadri ambao ni: padri Albert Mligo, Eventius Mdendemi, Gilbert Msaudzi na Paulinus Mligo.





Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU