ACHENI UKRISTO LEGELEGE-ASKOFU NZIGILWA



ASKOFU  Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar  es  salaam Mhashamu Euzebius Nzingilwa ,amewakumbusha  wakristo  wote  kuwa Yesu  Kristo havutiwi  na ukristo legelege, hivyo kila mtu anapaswa  kuwa chumvi  na nuru kwa wengine kwa kuyaishi vyema maisha ya kiimani.
Akizungumza  kwenye  mahubili  ya ibada  ya  misa takatifu ya hija  ya Umoja wa Wanaume Katoliki (UWAKA)  kijimbo  iliyofanyika Bagamoyo, Askofu Nzigilwa amesema Bagamoyo  ni mahali  pa kufukuza  giza na kuonyesha  njia itakayomfanya  mkristo ajue  wapi  akanyage  na  wapi asikanyage.
“Ninyi  ni chumvi  na  nuru  ya ulimwengu, itumieni  karama  hiyo kuangaza mwanga  palipo  na giza, kila  mmoja  anatakiwa  kujiuliza  tangu asubuhi hadi  jioni  amezuia  maovu  kiasi gani au kwanini  amekuwa  chanzo  cha  maovu  na si kukasirika  wala  kukunja ndita  za uso, bali upole na unyenyekevu uchukue hatamu kwa maana unyenyekevu haupimwi kwa action bali  hupimwa kwa reaction”.  
Kwa  upande  wake Mwenyekiti wa UWAKA Jimbo  Kuu Katoliki Dar  es Salaam  Amedeusi  Moshi amemshukuru Askofu, mapadri  na watawa wote  kwa ujumla  waliotoka  parokia mbalimbali na  kushiriki  pamoja  katika hija hiyo huku akiwataka  wanaume katoliki  kila parokia kuchangia  shilingi  laki tano (5) kwa ajili  ya  maboresho ya wafia dini  kituo cha hija cha Pugu Jjimbo Kuu Katoliki Dar  es  salaam.
Kwa upande  wake Katibu  wa UWAKA Jimbo  na taifa, Julius Kansonso amesema nia  hasa ya hija ya  Bagamoyo  ilikuwa ni kuwaombea  wanaume  wote ili watambue  na kuuishi  kwa vitendo wajibu  walionao kwa Mungu, kwa umma, kwa Kanisa na kwa  familia.





Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU