BREAKING NEWS: ASKOFU CASTORY MSEMWA WA JIMBO KATOLIKI TUNDURU MASASI AFARIKI DUNIA



Msiba mzito

Na Bernard James, DSM.

JIMBO Katoliki Tunduru Masasi limempoteza Askofu wa Jimbo hilo Mhashamu Castory Msemwa( katikati pichani)  aliyefariki leo majira ya saa 7 mchana nchini Oman.

Kwa mujibu wa Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi, Padri Jordan Liviga, Askofu Msemwa amefariki dunia akiwa mjini Muscat (Oman), akiwa safarini kwenda nchini India kupata matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

“Amefia nchini Oman wakati akienda kupata matibabu nchini India. Akiwa nchini humo amezidiwa ghafla na kupoteza fahamu, hadi umauti ulipomkuta.”

Marehemu Msemwa amekuwa na tatizo la kiafya kwa kipindi cha miaka miwili, na amekuwa akipata tiba mbalimbali na kuendelea na utume kama kawaida.

Aliondoka nchini siku ya Jumatano wiki hii kuelekea nchini India kwa matibabu kabla hajafariki dunia.

Padri Liviga amebainisha kuwa utaratibu wa kuuleta nchini mwili wa marehemu Askofu Castory Msemwa siku ya Jumapili Dar es Salaam unafanyika. Taarifa zaidi za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadaye.

Askofu Castory Paul Msemwa amezaliwa mwaka 1955 katika kijiji cha Kitulira, Parokia ya Matola Jimbo Katoliki Njombe. Alipata elimu ya msingi katika shule ya Motola, kisha Sekondari katika Seminari Kuu ya Peramiho ambapo alisomea Falsafa na Teolojia kati ya mwaka 1981 na 1987. Alipata daraja ya Upadri tarehe 7 Juni 1987. Amekuwa Paroko Msaidizi, Kiongozi wa vijana parokiani jimboni Njombe, mwalimu na amesoma katika Chuo cha Teresianum Pontifical College for Spirituality huko Roma na kuhitimu mwaka 1996. Alipata Daraja ya Uaskofu tarehe 30 Januari 2005 kisha kusimikwa kuliongoza Jimbo Katoliki Tunduru Masasi tarehe 25 Agosti 2005.

Mwenyezi Mungu ampumzishe pema mbinguni, Amina.


Comments

  1. Raha ya milele umpe EE Bwana Na mwanga wa milele umuangazie astarehe kwa amani. Amina

    ReplyDelete
  2. Raha ya milele umpe eeh Bwana apumzike kwa amani amina

    ReplyDelete
  3. Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie. Amina

    ReplyDelete
  4. Raha ya milele umpe eee Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie, apumzike kwa amani. Amina

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU