AMUCTA KUONGEZA UFAULU WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU





CHUO Kikuu kishiriki cha Askofu Mihayo Tabora AMUCTA na shirika toka nchini Uholanzi la KENTALIS wameendesha semina kwa walimu 25 wa shule za Sekondari ndani ya Manispaa ya Tabora kwa ajili ya watoto wenye matatizo ya kusikia na kuongea hivi karibuni Tabora.
Akiongea na Blogi hii juma hili, Mkurugenzi wa Kitivo cha Elimu Dr. Sr. Sophia Mbilije amesema chuo na shirika la Kentalis wameamua kutoa semina hiyo  kwa walimu wa sekondari ili kusaidia kuinua ufaulu wa watoto wenye tatizo la kusikia na kuongea.
Aidha katika semina hiyo wameandaa mtaala ambao watauweka katika kanzi data ili walimu na wanafunzi wote katika shule 19 za Tanzania zenye watoto wenye mahitaji maalumu waweze kupata ujuzi utakaowasaidia kujipatia elimu.
Katika Kanzi data hiyo walimu wamefundishwa kuweka, kuchukua na kutumia picha, michoro, na vielelezo vingine lengo likiwa kuwasaidia watoto hao wenye matatizo ya kusikia na kuongea waweze kuelewa mada zinazofundishwa madarasani na hatimaye ufaulu wao uweze kupanda.
Aidha Dr. Sr. Mbilije amesema wao na shirika hilo la Uholanzi wamelenga wanafunzi wa kidato cha kwanza na nne katika masomo ya sayansi, hii ikienda sambamba na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano yaani Tanzania ya viwanda.
Walimu waliopata bahati ya kupata semina hiyo ni kutoka shule za sekondari ndani ya Manispaa ya Tabora na chuo cha ualimu Tabora (T.T.C).
Semina hiyo ilihudhuriwa na wahadhiri  na wahadhiri wasaidizi wa chuo kikuu cha AMUCTA-Tabora ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na wawezeshaji toka ndani na nje ya Tanzania.
Zoezi hilo litakuwa endelevu katika Mkoa wa Tabora na hasa lengo kuu likiwa kuandaa wataalamu wa masomo ya sayansi hususani watoto wenye mahitaji maalumu.




Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU