UGONJWA WA MARBURG NCHINI: TAHADHARI YATOLEWA
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), mnamo tarehe 19 Oktoba 2017 kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda tangu tarehe 17 Octoba, 2017. Maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo ni Wilaya ya Kween, Kanda ya Mashariki ya nchi, ambayo inapakana n nchi ya Kenya. Hadi kufikia tarehe 19 Oktoba 2017, watu 4 walikwishapata maambukizo ya ugonjwa huo, ambapo wawili kati yao wamepoteza maisha. Wizara inatoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi katika mikoa yote ya Tanzania, hususan kwa wale wanaoishi katika mikoa ambayo inapakana na na nchi ya Uganda (Mikoa ya Mara, Mwanza na Kagera). Ugonjwa wa Marburg unafanana sana na ugonjwa wa Ebola. Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Marburg vinajulikana kama “Marburg Virus”, navyo vipo katika jamii moja na virusi vinavyosababisha Ebola (Ebola virus)....