“WATAWA MJIDHATITI KUJENGA MAHUSIANO KATI YENU, MAASKOFU, KANISA”
WIto umetolewa kwa watawa wa kike kutoka kanda ya Afrika
Mashariki na kati kuishi maisha yao ya wakfu kwa umojana maaskofu, mapadri,
ndani ya jumuiya zao na jamii inayowazunguka.
Hayo
yamebainishwa na Mwadhama João Kardinali
Bráz de Aviz, Rais wa Baraza la Kipapa la Maisha ya waliowekwa wakfu (CICLSAL) katika Mkutano Mkuu
wa 17 wa Umoja wa Watawa wanawake Afrika Mashariki na kati uliofanyika katika
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Kurasini jijini Dar es Salaam kuanzia
August 27-31 mwaka huu.
“Kusanyiko
hili la watawa ni fursa yetu sote kuwa pamoja, kushirikishana karama zetu,
changamoto zetu ili tukuwe pamoja kama wawekwa wakfu katika Kanisa.
Kardinali
Bráz de Aviz ambaye awali alifungua mkutano huo kwa Ibada ya Misa Takatifu
alitaka watawa waangalie changamoto zao za sasa kama wanajiandaaje na kuishi
maisha mapya baada ya mkutano huo kwani wato wa Baba Mtakatifu Fransisko kwa
watawa na kwa Kanisa ni kujitakatifuza kwa kufanya mang’amuzi mapya ya maisha
ya wakfu,” amesisistiza Karidinal Bráz de Aviz.
Amewataka
watawa watathmini mahusiano yao na viongozi wa Kanisa hususani Maaskofu na wote
wenye mamlaka katika Kanisa akiwataka warejee waraka wa Iuvenescit Ecclesia uliotolewa na Kongrigasio ya uenezaji Injili.
“Baba
Mtakatifu amesisitiza kongrigasio ya CICLSAL na kongrigasio ya Maaskofu kupitia
na kufanya marejeo ya waraka wa Mutae relationes’ (Mutual Relations).
Nyaraka
zote mbili zinazungumzia mahusiano thabiti kati ya Maaskofu na watawa (wawekwa
wakfu) kwa ajili ya kujenga umoja katika maisha ya kiroho, kushirikishana
karama ili kuliendeleza Kanisa,”
amesisitiza.
Amesema
ni wakati mwafaka wa kufanya tathmini kuanzia mtu binafsi, jumuiya , shirika na
umoja wa mashirika kuanza maisha mapya bila woga ili kuendeleza karama zao
muhimu ndani ya Kanisa.
“Zipo
baadhi ya changamoto ambazo zimo ndani ya jumuiya za watawa ikiwemo utengano.
Utakuta baadhi ya watawa wanaunganika huku wakimtenga mtawa mmoja ndani ya jumuiya
ambaye anabaki mpweke.
Inawezekana
wakaenda hata safari na kufanya shughuli zao na kumwacha mtawa mmoja akiteseka
kisaikolojia ndani ya jumuiya. Hii inaweza kumfanya akate tamaa, kusononeka na
kutopata mazingira chanya ya kuishi wito wake wa utawa.
Ndiyo
maana ninasisitiza umoja ndani ya jumuiya zetu za kitawa ili kuunganisha karama
zenu na kuishi kwa furaha maisha ya kumtumikia Kristo,” amesema Kardinali huyo.
Kardinali
de Aviz ameeleza changamoto nyingine ya watawa kuacha ,maisha ya wakfu akisema
si jambo la kuchukuliwa kawaida bali jitihada ziwekwe na wakuu wa mashirika
kuanzia ngazi za kitaifa na kimataifa.
“Walezi
lazima wawe makini kutoa malezi yanayoheshimu na kuthamini mila na desturi
mbalimbali za vjana pamoja na upana wa maisha ya kizazi cha sasa.
Kama
hakuna uwiano kati ya teolojia na utaalmu katika mafunzo matokeo yake ni kukosa
malezi yakini, nidhamu na maisha ya wakfu.
Lazima
wanaolea yaani walezi wawe na malezi na utaalamupamoja na teolojia ya kulea
wengine. Mlezi awe na malezi endelevu ndipo awalee wengine. Kadhalika wamama
wakuu na uongozi mzima lazima wapate malezi endelevu ili kuweza kulea
wanashirika.
Amesisitiza
pia suala la utawala ndani ya mashirika ya wawekwa wakfu. Kuwe na majadiliano
katika kuongoza mashirika ya kitawa ili kuwa na maamuzi ya pamoja badala ya
kiomgozi kutoa amri kwa walio chini yake ama kuwatenga kimamlaka.
Hata
hivyo Kardinali de Aviz amesema ameridhishwa kushiriki mkutano huo wa Watawa
(ACWECA).
Amesema
amaguswa na liturujia ya Misa Takatifu hapa Tanzania ambayo ilimfanya asali
mara mbili kwani niliturujia hai yenye utamadunisho ndani yake.
Comments
Post a Comment