PAPA FRANSISKO-ZIARA YA KOLOMBIA IMEKUWA YA TIJA


Siku zilizopita kama mjuavyo  nimemaliza ziara ya kitume huko Colombia. Kwa moyo wote ninamshukuru Bwana kwa zawadi kubwa, na kwa njia hiyo ninarudia kutoa shukrani zangu kwa Rais wa Jamhuri aliyenipokea kwa ukarimu mkubwa, Maaskofu wa Colombia waliofanya kazi sana kuandaa ziara hiyo ma  kama vile wote wenye madaraka ya nchi pia wote walioshirikiana kufanikisha ziara hiyo. Ni maneno  ya utangulizi wake Baba Mtakatifu Francisko Jumatano 13 Sepemba wakati wa kateksi yake kwenye viwanja vya Mtakatifu Petro, akielezea kwa ufupi juu ya ziara yake nchini Colombia aliyoanza tarehe 6 na kurudi Vatican tarehe 11 Septemba.
Anawashukuru kwa namna ya pekee watu wa colombia waliompokea kwa ukarimu mkubwa na furaha , anasema,  ni watu wenye furaha kubwa pamoja na mateso mengi lakini ni wenye furaha na matumaini. Kilichotoa mshangazo kwake  katika miji yote ni kuona baba na mama wakiwa na watoto wao,waliamasha watoto hao ili Papa awabariki, lakini zaidi ni ile ya kuonesha kuwa hawa ni watoto wetu ambao ndiyo matumanini yetu. Baba Mtakatifu anafikiri kuwa, watu wenye wezo wa kuzaa watoto wengi, wanao uwezo wa kujidai na kuwa na matumanini ya  wakati hujao na kwa njia hiyo alipenda sana tendo hilo.

Katika  ziara yake hiyo, kwa namna ya pekee anaelezea ,alisikia kuwa papa wawili waliwahi kutembela nchi ya Colombia Mwenye heri Paulo wa VI mwaka 1968 na Mtakatifu Ypohane Paulo  mwaka 1986, na kwamba ziara yake hiyo ni mwendelezo wa nguvu unaongoza na Roho  ambaye anaongoza hatua za watu hawa wa Mungu katika njia yao ya kihistoria. Kauli mbiu ya ziara ilikuwa hebu tufanya hatua ya kwanza kwa lengo la kudumisha machakato wa mapatano ya nchi ya Colombia katika kuelekea uhuru baada ya kukaa karibu muhongo wa vurugu za ndani , ambazo zimepanda mateso na uadui na kuongeza majeraha ambayo yanakuwa vigumu kupona. Lakini kwa msaada wa Mungu safari hiyo imeanzishwa. Katika ziara yake, Baba Mtakatifu anaongeza kuwa, amependelea kubariki jitihada hizo za watu na kuwahimarisha katika imani na matumaini na kupokea ushuhuda wa ambao ni utajiri mkubwa katika utume wake kwa ajili ya Kanisa. Anasisitiza kuwa ushuhuda wa watu hawa ni utajiri wa Kanisa zima.
Nchi ya Colombia kama ilivyo sehemu kubwa za nchi za Amerika ya Kusini, ni nchi yenye kuwa na mizizi ya nguvu ya kikristo. Na hiyo inajionesha katika uchungu uliotokana na maafa ya vita yaliyoikumba, lakini kwa wakati huo huo, inatoa uhakikia wa ujenzi wa amani na msingi thabiti utokanao na kiini cha matumaini yasiyo shindwa. Ni wazi kwamba shetani alitaka kugawanya watu hawa na kuharibu kazi ya Mungu, lakini zaidi inaonekana wazi kwamba upendo wa Kristo na huruma yake isiyo na kikomo ni yenye nguvu zaidi ya dhambi na mauti. Baba Mtakatifu anaendelea kusema, ziara hiyo ilikuwa ni kupelekea baraza za Kristo , baraka za Kanisa katika utashi wa mashi na amani itokayo katika moyo wa Taifa lile. Baba Mtakatifu anasema ameweza kuona katika macho ya maelfu na maelfu ya watoto na vijana waliojaza kiwanja cha Bogota na  ambao alikutana nao kila mahali alipokwenda , akiona nguvu za maisha lakini ikiwa ni wingi wa nguvu  za asili yenyewe kwasababu anasema, nchi ya Colombia ni nchi ya pili ulimwengumi kutokana na  uwepo wa viumbe hai.
Siku ya maombi ya maridhiano ilifanyika huko Villavincencio. Baba Mtakatifu anaeleza; Asubuhi kulikuwa na ibada kuu ya Misa Takatifu ikiwa pamoja na kuwatangaza mfiadini Askofu Jesús Emilio Jaramillo Monsalve, na  Padre Pedro María Ramírez Ramos. Mchana ilifanyika liturujia ya maridhiano , wakiwa na ishara ya Kristo kilema kama  watu wake kwa maana ya msalaba usio kuwa na   mikono wala miguu  huko Bocaya.  Kutangazwa wenye heri mashaidi , unakumbusha kwamba amani imesimikwa katika msingi na hasa juu ya damu ya mashaidi wengi wa upendo, ukweli na haki. Vilevile  hata wafia dini wa kweli waliuwawa kwa ajili ya utetezi wa imani yao, kama hao mashidi waliotangazwa wenye heri. Kusikiliza maadishi ya historia yao yalitoa  msisimko wa kweli hadi kufika kutoka  machozi ya uchungu na furaha pamoja. Mbele ya masalia ya mashahidi hao, nyuso  za watu watakatifu na waamini wa Mungu wa Colombia,walijisikia uzalendo wao wenye nguvu;  wakati huo huo  uchungu  kwasababu ya  kufikiria waathirika wengi, lakini hata furaha kwa ajili ya huruma ambayo Mungu anawakirimia  wale wanao mtegemea.
Baba Mtakatifu Francisko anasema, katika zaburi  iliyosoma mwanzo imesikika ikisema fadhili zake na uaminifu vitakutana , uadilifu na amani vitaungana (Zab 85,11). Ndani ya kipengele hicho cha  zaburi ndimo kuna utabiri ambao ulijitokeza siku ya Ijumaa nchini Colombia, ni utabiri wa neema ya Mungu kwa watu waliopata majeraha ili waweze kufufuka na kuanza kutembea katika maisha mapya. Maneno hayo yaliyo jaa unabii wa neema yalionekana katika historia na ushuhuda ulio tolewa kwa niaba ya wengi walio athirika na kujeruhiwa roho zao , lakini kwa neema ya Kristo wamewezea kujikomboa wenyewe na kufungua makutano ya msamaha na maridhiano.
Huko Medellin Baba Mtakatifu anaendelea kusema, ilikuwa ni ziara inayojikita katika kaulimbiu ya wa maisha ya kikristo kama mfuasi:wito na utume. Kwa namna hiyo anasema, iwapo mkristo anajibidisha kwa kina hadi mwisho katika safari ya kumfuasa Kristo Yesu ,ni wazi kwamba  anakuwa kweli chumvi, mwanga na chachi ya ulimwengu na matunda mengi yanaonekana. Moja ya matunda hayo anasema, baba ni Hogares, maana yake nyumba za watoto walio athiriwa na vita , ambapo watoto hao wanaweza kupata familia mpya na mahali ambapo wanapendwa , wanapokelewa, wanalindwa na kusindikizwa. Matunda mengine zaidi ni wito wa maisha ya upadre na watawa . Baba mtakatifu anasema aliwaza kuwabariki na kuwatia moyo na zaidi  kuwa na furaha isiyo sahaulika, ya kukutana wao wakiwa na wazazi wao wote.
Na misho wa ziara yake ilikuwa ni Cartegna , mji wa Mtakatifu Petro Claver mtume wa watu watumwa. Kauli mbiu ya katika eneo hilo iliongozwa na uhamasishaji wa mtu na haki zake msingi. Mtakatifu Peter Claver kama vile Mtakatifu wa hivi karibuni Maria Bernarda Bütler, walitoa maisha yao kwa ajili ya maskini na walio baliguliwa, kwa njia hiyo wameonesha njia ya kweli ya mapinduzi na siyo ya kiitikadi,  bali njia ya kiinjili inayoleta kweli  uhuru wa binadamu na jamii  kuondokana  na  utumwa wa jana ,japokuwa kwa bahati mbaya hata leo hii.
Amemalizia Baba Mtakatifu kuelezea kwa ufupi ziara yake ya kitume akisema, kwa mara nyingine tena anawawakabidhi watu wote wapendwa wa Colombia kwa mama Maria mama yetu wa Chiquinquirá aliyeweza kumtolea heshima  katika Kanisa Kuu jijini Bogota. Kwa msaada wake, kila mtu nchini Colombia aweza kufanya kila siku hatua ya kwanza kuelekea kwa ndugu kaka na dada, ili wote  waweze kujenga kwa pamoja kila siku amani ya upendo, katika haki na ukweli.
Hisani ya:
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI