Askofu Ndorobo: Wazazi zingatieni sala za familia

n Na Philipo Josephati, Dar es Salaam
ASKofu wa Jimbo Katoliki  Mahenge Mhasham Agipiti Ndorobo, amewataka wazazi kusisitiza sala za pamoja ndani ya familia ili kujenga msingi wa imani ambayo inaanzia kwenye Familia.
Askofu Ndorobo ameyasema hayo wakati wa Ibada ya Misa Takatifu alipokuwa akitoa Sakramenti Takatifu ya kipaimara kwa vijana 88 katika Parokia ya Mwenyeheri Anwarite Makuburi jijini Dar es Salaam.
Amesema kuipeleka Injili mbele inawapasa waamini kwa pamoja kulingana na mazingira yao kuwajibika kuimarisha imani Katoliki kwani si kazi ya mapadri na maaskofu tu kutangaza Injili.
Amesema kila mmoja ana karama zake alizojaliwa na Roho Mtakatifu hivyo ni vyema akazitumia kujenga msingi imara wa imani na kujenga taifa adilifu, lenye heshima na lenye watu wacha Mungu.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU