HAKUNA UKRISTO BILA MSALABA - ASKOFU NZIGIRWA

n NA PHILIPO JOSEPHAT DAR ES SALAAM

ASkofu Msaidizi wa Jimbo  Kuu Katoliki  Dar es Salam, Mhashamu Euzebius Nzigilwa amewataka wakristo kutambua kuwa hakuna kuitangaza injili ya Yesu Kristo  bila msalaba..
 Akizungumza kwenye sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba iliyofanyika katika Kituo cha Hija Pugu jijini Dar es Salaam, Askofu Nzigilwa amesema nyakati za hivi karibuni wamejitokeza watu mbalimbali ambao huihubiri injili bila msalaba na kuwaeleza watu kuwa endapo wataungana nao watapata utajiri, watapona magonjwa na kupata mali nyingine mbalimbali zikiwemo fedha .Amewataka wakristo kuwa makini kwa kumfuata Kristo anaye tangazwa kwa Msalaba Mtakatifu .
Ameongeza kuwa hapo zamani mtu aliyesulubiwa msalabani alionekana mwenye dhambi na kudharauliwa, lakini kupitia msalaba huo huo umekuwa mkombozi wa ulimwengu nzima. Wakati huo huo Askofu Nzigilwa ametoa salamu kutoka kwa Mwadhama Polycarp Kardnali  Pengo  kwa  waamini na kuwaambia kuwa,  hakuweza kuungana nao kwa sababu ya ushauri wa madaktari wanaomuhudumia kumtaka apumzike.
Hija hiyo  iliwakutanisha wakristo wote wa Jimbo Kuu  Dar es Salaam kutoka parokia mbalimbali akiwepo  Spika Mstaafu Mheshimiwa Anna Makinda.   


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU