Mvimwa wapata Abate Mpya
WATAWA wa shirikala Mtakatifu Bernediko wa Abasia ya Roho
Mtakatifu Mvimwa WAMEPATA Abate mpya
Padri Pambo Martin Mkorwe OSB.
Akiongoza Ibaada ya Misa Takatifu kumuombea
Abate Pambo Askofu wa Jimbo
Katoliki Sumbawanga Mhashamu Damian
Kyaruzi amemuasa Abate Pambo kufuata mfano wa Mt. Pio wa X Papa, anayekumbukwa
August 21 ambaye alijitoa kulihudumia Kanisa la Mungu bila kujibakiza.
Akiwashukuru wananchi na waamini wa jimbo la Sumbawanga abate Pambo
OSB amemshukuru askofu na waamini kwa
mapokezi na kumuombea na kuahidi kufanya kazi kwa moyo kadiri ya matakwa ya
Mama Kanisa.
Abate Pambo atasimikwa August 26 mwaka huu katika Makao Makuu ya Shirika
Mvimwa Parokiani Kate jimboni Sumbawanga .
Aidha Abate huyo amesema anaongozwa na kauli mbiu DUC IN ALCUM (Tweka mpaka kilindini)
Historia fupi Abate
Pambo Martin-Angelica Mkorwe OSB
Abate Pambo Martin-Angelica Mkorwe alizaliwa tarehe 15/08/1975 huko Uwemba
Mission, katika jimbo la Njombe, kwa baba Martin Mkorwe na Mama Angelica
Samligo. Alipata Sakramenti za Ubatizo, Ekaristi Tatakatifu na Kipaimara katika
Kanisa la Mtakatifu Rafaeli - Uwemba.
Kuazia mwaka 1983 – 1989 alipata elimu ya msingi katika shule za
Myangayanga – Jimbo la Mbinga, Uwemba – Jimbo la Njombe na mwisho Ihalula –
Njombe. Mwaka 1990 – 1996, akapata elimu ya sekondari katika Sekondari ya
Njombe (NJOSS), na Irambo katika Jimbo la Mbeya.
Mara baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1996, alianza rasmi safari
ya maisha ya Kitawa. Tar 11.07.1998, alifunga nadhiri za kwanza Mvimwa
Monasterini. Kuanzia mwaka 1998 – 2005alipelekwa masomoni Morogoro kwa ajili ya
majiundo ya Falsaka na Tauhidi katika Taasisi ya Wasalvatoriani.
Tarehe 22/08/2004, alifunga nadhiri za Daima – Mvimwa Abasiani. Tarehe 23
Octoba 2004, alipewa Daraja Takatifu ya
Ushemasi na Mhashamu Askofu Telesfor Mkude huko Salvatorian Institute –
Morogoro. Tarehe 10/07/2005, alipewa Daraja Takatifu ya Upadri katika Parokia
ya Kristo Mfalme - Sumbawanga na Mhashamu Damian Kyaruzi, Askofu wa Jimbo
Katoliki Sumbawanga.
Mara baada ya kupadirishwa, alitumwa kufanya kazi katika Parokia ya Kristo
Mfalme Sumbawanga mjini, kama Paroko
Msaidizi. Kuanzia mwaka 2008 – 2013, aliwekwa kuwa Paroko katika Parokia
hiyohiyo ya Kristo Mfalme Sumbawanga,
na wakati huohuo alitumikia kama Mkuu wa Idara ya Liturujia – Jimbo na Padri wa Kiroho wa
Gereza la Sumbawanga mjini.
Tarehe 1 Julai 2013, alitumwa Roma kusomea Shahada ya Uzamili katika
Sheria za Kanisa, ambako alihitimu mwezi Juni 2016. Tarehe 14/10/2016 Mkutano
Mkuu wa XXI wa Shirika, uliyofanyika huko Sankt Ottilien - Ujerumani,
ulimchagua Padri Pambo OSB kuwa Katibu wa Shirika la Wabenediktini
Wamissionari, na hivyo akahamishia makazi yake huko Ujerumani.
Ametumikia wajibu huo kwa muda wa miezi minane tu, ambapo tarehe 7/6/2017
jamii ya Wamonaki wa Mvimwa walimchagua kuwa Abate wa III wa Abasia ya Roho
Mtakatifu Mvimwa.Tarehe 25/8/2017, ameungama Imani na kula kiapo cha Uaminifu
kwa Mama Kanisa Mtakatifu na tarehe 26/8/2017, Mhashamu Damian Kyaruzi amempa
Baraka ya Uabate huko Abasiani Mvimwa.
Abate Pambo Martin Mkorwe osb ambaye Kauli-mbiu:ni Motto DUC IN ALCUM (Tweka Mpaka Kilindini)
Lk. 5:4 amekuwa ni abate wa tatu katika nyumba ya Abasia ya Roho Mtakatifu
Mvimwa akitanguliwa na Abate Mstaafu Denis Ndomba OSB na hayati Abate Basil
Ngaponda OSB.
Comments
Post a Comment