UJUMBE WA VATIKANI KUHUDHURIA JUBILEI YA UPADRI DODOMA
KUELEKEA kilele cha Jubilei ya Miaka ya
upadri Tanzania, imethibitika kuwa katika sherehe hiyo Mkuu wa Idara ya
Uinjilishaji Vatikani Kardinali Fernando Filoni atawakilishwa na Katibu
Mwambata na Rais wa Mashirika ya Kitume ya Kipapa, Askofu Mkuu Protas Rugambwa.
Hayo yamebainishwa na Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya, katika mwaliko wake kwa
maaskofu wa kuhudhuria kilele cha jubilei hiyo itakayofanyika Agosti 15 jimboni
Dodoma.
Askofu Kinyaiya pia ameeleza kuwa katika
sherehe hiyo Balozi mpya wa Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu Marek Solczynski
anatarajiwa kujitambulisha rasmi kwa waamini nchini.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa kwa
ajili ya maadhimisho hayo, Misa Takatifu ya uzinduzi wa jubilei hiyo inatarajiwa
kufanyika Agosti 14 na kuongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma Mhashamu
Joseph Mlola, na baada ya misa zitafuata semina mbili zitakazowezeshwa na
Askofu Desderius Rwoma wa Jimbo Katoliki Bukoba na Padri Titus Amigu wa Jimbo
Katoliki Lindi.
Misa Takatifu ya kilele cha jubilei
inatarajiwa kuongozwa na Askofu Mkuu Protas Rugambwa ambapo pia baada ya misa
atabariki jiwe la msingi la kikanisa katika makao mapya ya Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania (TEC) jimboni Dodoma.
Comments
Post a Comment