"DUMISHENI UPENDO" ASKOFU MLOLA

Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma na Mlezi wa Umoja wa Mapadri Tanzania (UMAWATA) Mhashamu Joseph Mlola amewataka mapadri nchini kuimarisha upendo baina yao pia  wananchi wote ili Taifa liendelee kuwa na amani upendo na mshikamano hali itakayochochea ukuaji wa maendeleo. Ameyasema hayo muda si mrefu katika adhimisho la Misa Takatifu ya uzinduzi wa Kilele cha Jubilei ya Miaka 100 ya Upadri Tanzania Bara iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma. Kilele hicho kitafanyika hapo kesho(Jumanne).

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI