Padri awasisitiza waamini kuzithamini Kumbukumbu za Watakatifu
WAKRISTO
wote wametakiwa kuzipa umuhimu
na kuzisherehekea sikukuu
mbalimbali za watakatifu wa
Kanisa ikiwemo ile ya
Bikira Maria kupalizwa
mbinguni.
Wakiongea wakati
wa kusherekea sikukuu ya
kupalizwa Bikira Maria mbinguni, baadhi ya
wanajumuiya ya Bikira
Maria Mpalizwa wa Mbinguni wamesema kila
mkristo anapaswa kujua wajibu
wake wa sala
kwa kumuomba Bikira Maria awaombee
kwa mwanae Yesu.
Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo toka parokia
ya Kimbiji Dar es salaam
Joseph Kusandika amewataka
wakristo kupeleka sala
zao kwa Bikira
Maria ili wapate
amani ambayo italeta
mwanga mpya ndani
ya familia na jumuiya
zote.
Paroko
msaidizi wa parokia ya Kimbiji
padri Justus Lugayimkam aliyeongoza Misa hiyo ameeleza
juu ya mwanzo wa sikukuu
ya kupalizwa Bikira
Maria mbinguni. “Sikukuu ya
kupalizwa mbinguni Bikira
Maria ilitangazwa rasmi mnamo
mwaka 1950 na
Papa Pius wa
kumi na mbili,
na mnamo karne
ya 6,550 BK ilijulikana
kama sikukuu ya Domisiyo
wakati mnamo karne
7-8 ikajulikana kuwa
sikukuu ya Somisiyo,
kuanzia karne ya 8-21
na hadi leo inajulikana
kuwa ni sikukuu
ya kupalizwa Bikira
Maria mbinguni,” amesema padri Lugayimkam.
Aidha padre
Lugayimkam ameongeza kuwa zipo
sababu kuu nne
zinazoeleza kupalizwa kwa Bikira
Maria mbinguni, sababu ya
kwanza ni kwamba
Bikira Maria alikingiwa
dhambi ya asili,
ya pili Bikira
Maria alidumu katrika ubikira
wake, tatu Bikira
Maria ni Mama wa
Mungu na ya mwisho ni
ukaribu wake na mwanaye
Yesu Kristo.
Wakati
huohuo wakristo wote wanatakiwa kuishika, kuitetea imani
bila kujali adha
au matatizo ambayo yatawapata.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni katika
kigango cha Mbutu
Kigamboni Kimbiji Dar
es salaam na
padri Justus.
“Mkristo
anapoiacha imani moja kwa
moja anaingia kwenye
matatizo makubwa
yatakayomtenga na Mungu, kilicho mfanya Petro kuzama kwenye
bahari wakati Yesu
alipomuita atembee juu ya
maji ni kukosa
imani, hofu na mashaka ya upepo
uliokuwa ukivuma baharini na
kusababisha kuanza kuomba
msaada kwa Yesu amuokoe. Katika sura
hiyo waamini wanapaswa
kutambua kuwa kwa
sayansi ya mwanadamu ni vigumu
kutembea juu ya maji, lakini ndiye
mwanasayansi namba moja katika
maisha yetu yote ,hivyo
inampasa kila muamini kumfuata
Kristo na kuilinda
imani itupatiayo wokovu.”
Comments
Post a Comment