Kampuni iliyomsadia Trump, yamfanyia kazi Rais Kenyatta
KAMPUNI moja ya data ya
mitandaoni iliyomfanyia kazi Donald Trump na ambayo ilitumika katika kampeni za
Brexit sasa imeripotiwa kumfanyia kazi rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Lengo la Cambridge
Analytica ni wazi. Katika Mtandao wake kampuni hiyo inasema inatumia data
kubadili tabia ya wateja wake.
Kampuni hiyo
iliokodishwa na kundi la kampeni za rais Trump imepongezwa kwa ushindi wa rais
huyo.
Kampuni hiyo
inanunua na kukusanya data kuhusu wapiga kura ikiwemo historia ya utumizi wao
wa mtandao, mahali walipo pamoja na ‘Likes’ zao {wanachopenda} katika mtandao
wa facebook.
Katika mtandao wake,
Cambridge Analytica inadai kukusanya maeneo 5,000 ya data miongoni mwa wapiga
kura milioni 320 wa Marekani.
Zinapochanganywa
pamoja na utafiti unaofanywa , Cambridge Analytica inaweza kutumia data hiyo
kutoa ujumbe muhimu kwa wapiga kura.
Kwa sasa Cambridge
Analytica inafanya kazi Kenya , ikisaidia juhudi za kuchaguliwa tena kwa rais
Uhuru kenyatta.
Mnamo mwezi Mei ,
gazeti la The Star nchini Kenya liliripoti kwamba Chama cha rais Kenyatta,
Jubilee kimekodisha kampuni hiyo na
mwezi mmoja baadaye ,gazeti hilo hilo liliripoti kwamba Cambridge Analytica
ilikuwa ikifanya kazi katika ghorofa ya 7 ya jumba la makao makuu ya chama
hicho jijini Nairobi.
Cambridge Analytica
ilikataa kutoa tamko lolote kuhusu ripoti hizo kwa kitengo cha habari cha BBC
Trending, lakini shirika la Privacy International lilithibitisha kwamba liliona
habari kama hizo katika gazeti la The Star kufuatia duru kadhaa, na kusema kuwa
Cambridge Analytica inalipwa dola milioni sita kwa kazi yake nchini humo.
Cambridge Analytica
ilishirikishwa katika siasa za Kenya 2013 wakati kampuni hiyo ilipomsaidia
Kenyatta na chama cha National Alliance ambacho kilibadilika na kuwa Jubilee
Wakati wa kampeni za
mwaka huo kampuni hiyo ilichanganya data ya mitandaoni na tafiti 47,000.
Kulingana na mtandao
wa Analytica hatua hiyo iliisaidia kampuni hiyo kutengeza maelezo mafupi ya
mpiga kura wa Kenya na kutafuta mikakati ya kampeni inayolingana na mahitaji ya
mpiga kura mbali na hofu ya kuzuka kwa ghasia za kikabila.
Kenyatta alishinda
uchaguzi huo wa 2013.
Wakenya ni miongoni
mwa watu wanaotumia sana mtandao barani Afrika.
Idadi ya watu
wanaotumia simu za rununu nchini humo iliongezeka kutoka watu milioni nane 2007
hadi milioni 30, 2013 na asilimia 88 ya idadi ya watu sasa wanaweza kutumia
mtandao kupitia simu zao.
Baada ya kuhudumu
kama waziri wa habari na mawasiliano kutoka 2005 hadio 2013 , Bitange Ndemo
alikuwa mmoja wa viongozi waliosadia kupanua sekta ya teknolojia.
Alisema kwamba
mitandao ya kijamii ina jukumu kubwa katika kampeni za uchaguzi nchini humo.
‘’Inatoa njia ya
haraka ya kujibu propaganda za mpinzani wako’’ , alisema, mbali na kuwa mfumo
wa mawasiliano unaoweza kuwafikia vijana wengi.
Comments
Post a Comment