WAONYESHENI NJIA SAHIHI WAAMINI-ASKOFU MINDE
Askofu Minde amesema hayo katika mahubiri kwenye misa ya
kuhitimisha mkutano mkuu wa wajumbe
wa chama cha kitume cha Shirika
la Moyo Mtakatifu wa Yesu waliokutana jimboni katoliki Kahama.
Askofu Minde amesema
baadhi ya waamini wamekuwa wakikosa mwelekeo katika maisha yao na kuomba vyama
vya kitume kuwasaidia katika mambo ya
imani ya kanisa katoliki na kuwarudisha katika mwelekeo mzuri kuanzia ngazi ya
familia na jumuiya ndogondogo.
Aidha amesema uwepo
wa shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu ndani ya
kanisa kwa sala na maombezi linapaswa kupongezwa huku
akilihimiza kutunza usafi wa moyo
katika mambo ya uijilishaji, kuendelea zaidi na ibada zao na kulitangaza shirika ili waamini wa rika zote
waweze kujiunga nalo.
Viongozi wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu toka majimbo yote katoliki nchini ambao ni
wajumbe wa mkutano mkuu
wa Taifa wamekuwa na kikao
chao cha siku
tano jimboni Kahama ambapo pamoja
na kujadili maendeleo ya utume
wao pia wamefanya uchaguzi wa viongozi wa
kitaifa .
Viongozi wa kitaifa waliochaguliwa katika mkutano mkuu wa
shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu
ni Mwenyekiti Longinus Kagaruki ,
makamu mwenyekiti Christopher Mrope , Katibu mkuu ni Richard Mahundi , Katibu Msaidizi Ernesta
Mosha , Muweka Hazina Martina Kisaka na
muweka hazina msaidizi ni Fredrick Leonard.
Na Patrick Mabula , Kahama .
Comments
Post a Comment