MADHARA YA TETEMEKO BUKOBA:KANISA KATOLIKI LAATHIRIKA, MISAADA YAHITAJIKA
Sarah Pelaji, Dar es Salaam
BAADA ya tetemeko la ardhi kuukumba mkoa
wa Kagera, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini
ameeleza kuwa, Kanisa Katoliki limepata maafa na hasara ikiwemo kuharibika kwa
nyumba ya Askofu wa Jimbo hilo, Mhashamu Desiderius Romwa, nyumba yake
anayoishi, makanisa, shule zinazomilikiwa na Kanisa, Chuo Kikuu (SAUT) tawi la
Bukoba na nyumba za mapadri.
“Kwakweli si
Kanisa tu lililopata maafa bali jamii nzima. Nyumba nyingi zimeanguka, watu
analala nje, hawana makazi, wamefariki na kupata majeruhi.
Kwa upande wa
Kanisa hali ni mbaya maana Kanisa la kwanza kujengwa katika Mkoa wa Kagera la
Kashozi ambalo lilijengwa mwaka 1892-1897 limepata nyufa amabzo zinaweza
kusababisha Kanisa hilo likaanguka. Nyuma ya Askofu wa Jimbo huko Ntungamo nayo
imapata nyufa hadi amahamia kwenye kichumba ambacho kwakweli anajisitiri tu.
Mimi mwenyewe
nimehama kwenye nyumba yangu ya kuishi kwani imepata nyufa na vitu vimeharibika
hapafai kuishi. Nyumaba ya mapadri huko kashozi nayo imaharibika haifai kuishi
mtu hivyo mapadri wanalala nje kwenye magari,” ameeleza Askofu Kilaini.
Amezitaja baadhi
ya shule za Kanisa Katoliki zilizoharibika kuwa ni pamoja na shule ya wasichana
ya Hekima ambapo mabweni yameanguka, shule ya Ihungo iliyojengwa mwaka 1949
nayo imaharibika na kanisa lake limebomoka na nyumba ya mapadri.
Akizungumzia namna
ya kusaidia maafa hayo Askofu Kilaini amesema kuwa, kila Askofu anajaribu
kuweka mikakati ya namna anavyoweza kusaidia maafa hayo ili kufanikisha lile
linalowezekana kwa sasa.
Comments
Post a Comment