PAPA AIOMBEA AMANI GABON



Papa Fransisko akiongea na mahujaji na watalii St Peter’s Square amesema anaungana na Maaskofu katika nchi ya Gabon kuvishawishi vyama kukataa vurugu na kuwa na lengo moja la mafanikio kwa nchi yao. Pia amewahimiza watu wote hususani wakatoliki kuwa wajenzi wa amani katika kufuata sheria, majadiliano pamoja na undugu.
Nchi hiyo imekuwa katika mgogoro wa kisiasa mara baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni, rais Ali Bongo na mpinzani wake mkuu Jean Ping wakishindwa kuelewana kutokana na matokeo ya kura zilizopigwa.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI