JELA MAISHA KWA KUCHOMA MAKANISA BUKOBA
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoani Kagera imewahukumu kifungo cha maisha
watu watatu kwa makosa ya kula njama na kuchoma makanisa mbalimbali
mkoani hapa.
Mwendesha
Mashtaka wa Serikali, Emmanuel Manyere alisema licha ya hukumu hiyo,
bado watu hao watatu wanakabiliwa na kesi ya kukata makoromeo na mauaji
ya watu 16 ambayo inaendelea katika Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba.
Manyere
alisema watu hao watatu ambao ni Allyu Dauda, Rashid Mzee na Ngesela
Keya walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, mbele ya Hakimu Mkazi
wa Bukoba, Victor Biambo.
Alisema washtakiwa hao kwa pamoja wamekutwa na hatia ya kula njama na kuchoma makanisa 16 ya madhehebu mbalimbali mkoani hapa.
Hakimu
Bigambo alisema Mahakama imeridhishwa na ushahidi kutoka upande wa
walalamikaji na kutoa adhabu ya kifungo cha miaka saba jela kwa wote
watatu kwa kosa la kula njama na kifungo cha maisha kwa kosa la kuchoma
makanisa.
Wakati
huo huo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Augustino Ollomi
aliipongeza Mahakama kwa kutenda haki katika kesi hiyo pamoja na
kuwataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa polisi ili kukomesha
vitendo kama hivyo.
Licha
ya hukumu katika kesi hiyo namba 67, bado watu hao watatu wanakabiliwa
na kesi ya mauaji ya watu 20 katika maeneo mbalimbali mkoani humo
inayoendelea katika Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba.
Comments
Post a Comment