ELIMU IWE CHOMBO CHA KUMKOMBOA MWANADAMU
ASKOFU wa Jimbo Katoliki Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema kuwa, elimu ni chombo cha ukombozi kwa mwanadamu na iwapo ataikosa anapungukiwa uelewa na uwezo wa kuyatawala mazingira anamwoishi.
Askofu Ngalalekumtwa ameyasema hayo kupitia hotuba
yake iliyosomwa na Katibu wa Elimu Jimboni humo Padri Dkt. Pius Mgeni kwenye
kikao cha mameneja na wakuu wa shule zinazomilikiwa na Jimbo hilo uliofanyika
katika ukumbi wa kichangani senta ya vijana.
Mhashamu
Ngalalekumtwa amesema kwamba binadamu asiye na elimu hawezi kutoa mchango wake
kuindeleza familia ya mwanadamu (jumuiya).
“Kanisa
linatambua wajibu wake wa kumfanya mwanadamu afurahie ile zawadi na heshima
aliyopewa kama mwana wa Mungu, ndiyo sababu wamisionari wetu toka kuingia kwao
nchini mwetu walijenga na kuendesha shle katika ngazi mbalimbali, kuanzia elemu
ya awali, msingi, sekondari, vyuo vya
ufundi stadi na ualimu, hadi sasa tumefikia elimu ya juu.
Jimboni
kwetu utume kwa njia ya elimu unabebwa na parokia, watawa na hata vikundi
binafsi kazi ambayo siyo rahisi kwani ni sadaka nzito kuwa na rasilimali watu,
miundombinu na fedha za uendeshaji, samani, na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia.
Uchumi
wa leo umekuwa mgumu kwa wote, yaani wazazi na wamiliki wa shule..pamoja na nia
njema tunafikia wakati ambapo tunaelekea kukwama.
Elimu
inadai mpangilio katika sekta zote, ndiyo sababu serikali inaandaa sera ya
kuratibu elimu nchini. Nalo Kanisa kama
mdau linaandaa sera ya elimu ili misingi ya Injili izingatiwe” amesema na
kuongeza kuwa “ katika kutekeleza hilo Kanisa Katoliki nchini mwetu (T.E.C.)
linashirikiana na Makanisa mengine (C.C.T.) katika ile Tume ya Huduma za Jamii
za Kanisa (Christian Social Services Commision CSSC)”.
Mhashamu
Ngalalekumtwa amesema kwamba katika ngazi ya Jimbo wanaagizwa kuwa na sera
inayoratibu utekelezaji wa maagizo, maamuzi na makusudio au malengo ya elimu
kutoka ngazi za juu.
Katika
kikao hicho mameneja na wakuu hao wamepitia sura nane (8) za sera ya elimu
Jimbo la Iringa, pamoja na mambo mengine, Pd. Mgeni amewataka wamiliki hao
kuendesha shule zao inayoendana na kanuni, taratibu na sheria za Kanisa Katoliki.
Katika
kikao hicho washiriki hao waliunda kamati ya Elimu Jimbo, mwenyekiti wake akiwa
ni Pd. Pius Mgeni, katibu ni Francis Mwilafi na Mhazina ni Sr. Matrida Chuhila
wa Shirika la Wateresina wa Mtoto Yesu (CST).
Na Getrude Madembwe, Iringa.
Comments
Post a Comment