PAPA FRANSISKO AWAKUMBUSHA WABATIZWA


Mkristo ni lazima kusonga mbele na maisha kwa kuutunza mwanga wa imani, tulioupokea bure siku ya ubatizo wetu. Ni ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa mapema Jumatatu hii,  wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu  Marta ndani ya Vatican.  Katika homilia hiyo, ameonya  dhidi ya tabia mbovu mbalimbali zinazoweza kuufifisha  mwanga unaomulikia maisha safi ya kumtegemea Mungu. Ametaja baadhi ya tabia mbovu  kuwa ni pamoja na wivu, chuki , fitina na  kula njama dhidi wengine, na hasa dhidi ya wakarimu na watenda mema. Na kwamba, kitendo chochote kinachokuwa kinyume na  ubinadamu, hicho ni  kitendo cha giza, ni kitendo cha kishetani , au utendaji wa mafia kama inavyojulikana hapa Italia.
Papa ameeleza na kumhimiza kila mbatizwa kuuweka mwanga wa imani yake katika  kinara, mahali unapoweza onekana waziwazi  hadharani kupitia ushuhuda wa maisha,  kuuacha mwanga huo uangaze mbele ya watu wote.  Papa Francisko ametoa meelezo hayo akilenga katika somo Injili ya Siku, ambamo mnazungumzia juu ya  kudumisha mwanga wa imani hai, na hatari zinazoweza kuufifisha mwanga huo. Mwanga wa imani tuliopokea wakat iwa ubatizo , zawadi ya bure kutoka kwa Mungu.  Papa, alikumbusha pia kwamba wakati wa karne za mwanzo za Kanisa,  na bado katika baadhi ya makanisa ya Mashariki , ubatizo huitwa ” Nuru”.
Papa ameendelea kueleza kwa jinsi ilivyo kuwa vigumu kuuzima au kuufunika mwanga  huu, kwa kuwa mwanga huo ni  Yesu Kristo mwenyewe . Ndiyo maana Injili inatutaka kuuishi mwanga huu kikamilifu na si katika hali za nusunusu zisizoeleweka, kama ni Mkristo au la.  Ni lazima kuionyesha nuru ya kweli tunaipokea wakati wa ubatizo ,kumpokea Kristo mwenyewe ambaye ni upole, utulivu  na hai kamili, kwa sababu Yeye ni Bwana, na kwa mwanga huu hufukuza maisha ya giza.
Papa ameonya kamwe mbatizwa asiwe mbali na nuru hii, nuru inayomulikia fadhila na wema kwa ajili ya  wengine, ni mwanga usiowatakia wengine maovu , isipokuwa mazuri na mema yote , kwa sasa na hata kwa  siku za baadaye.
Papa ameeleza na kukemea tabia za kutaka kubishana tu wengine , mabishano yasiyokuwa na tij, isipokuwa kuchochea maovu na ubaya . Ameshauri iwapo kunajitokeza  mabishano au mjadala ju ya imani mbamo mtu haelewi kile anachofahamishwa, ni jambo jema, kusitisha mjadala huo,  katika hali ya utulivu na amani kuliko kung’ng’ana tu hadi kuzua ugomvi au mapigano. Kwa Mkristo ni jambo la busara, wakati huo wa mtafaruko wa mabishano,  bila kupoteza imani, kusamehe maongezi  kwa amani  bila ugomvi . Aliendelea kutoa ushauri wa kibaba, kwamba ni kukubali kusamehe bila kuufunika mwanga wa imani kwa kuhusudu ujeri wa wengine au kukatishwa kwa sababu ya mafanikio yao, kwa kuwa Bwana , huwondoa ujeri wa wanaokaidi, na hujeng aurafiki na wote wanaomridhia.
Papa amemalizia homilia yake kwa kumwomba  Roho Mtakatifu, awawezeshe  wote waliopokea  ubatizo, kutoanguka katika tabia hiii mbovu ya kutaka kuufunika mwanga wa ubatizo, mwanga kutoka kwa  Mungu, wenye kuwezesha kutenda mengi mema kwa ajili ya wote,  mwanga urafiki, mwanga wa upole, mwanga wa imani, mwanga wa matumaini, mwanga wa uvumilivuna wema owte.  mwanga wa wema.
TEC

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI