ASKOFU KYARUZI AHIMIZA MSAADA KWA WAHANGA WA TETEMEKO
Na Emanuel Mayunga
Sumbawanga
ASKOFU kwa Jimbo Katoliki la Sumbawanga
Mhashamu Damian Kyaruzi amewataka wakristo na watu wote nchini kuwasaidia
waanchi wa mkoa wa Kagera katika maafa waliyopata hivi karibuni kutoakana na
tetemeko la Ardhi lililosababisha vifo kadhaa, kuharibu majengo na mali.
Askofu Kyaruzi
ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la siku 8 la hija ya Mwaka wa Huruma
ya Mungu lililoanza Septemba 11 katika
viwaja vya Libori Center Manispaa ya Sumbawanga
na kuhitimishwa jumapili ya 18 Septemba mwaka huu katika mlima wa hija
maarufu kwa jina la Itwelele uliopo manispaa ya Sumbawanga.
Katika kongamano
hilo askofu Kyaruzi amesema kuwa katika nyakati hizi watu hawajali wala kuguswa
na matatizo ya wengine hasa wanaokubwa na maafa na ajali zinazosababisha vifo,
majeruhi na hata wengine kukosa makazi./ Baadhi wanaona kama si sehemu ya
maisha yao kwakuwa hayatokei sehemu walipo
‘Ndugu zangu
wakristo na watanzania wote tunapaswa tutambue kwamba, kuwa na huruma
hakuhitaji dini, huruma si ya kabila, huruma si ya taifa, sura, rangi, tajiri
au masikini bali ni hisia na mguso wa ndani ambao mtu anaona thamani ya
mwenzake katika mahitaji aliyonayo na kumsaidia kutatua au kuondoa kile ambacho
kinamfanya mwingine akose amani.
Tuwajali wenzetu
bila kujali tofauti zetu. Kwenye maafa pasiwepo siasa, ukabila wala matabaka. Huruma
ni kielelezo cha upendo’.
Aidha askofu
kyaruzi mwaka wa Huruma ya Mungu
unasisitiza kuomba huruma na kuhurumia wengine. Ndio maana dunia ya sasa ina
vita kila mahali lakini chanzo chake ni kukosa upendo, unyenyekevu na msamaha
kwa wengine.
“Dunia yetu vita
vimetawala baina ya taifa na taifa watu kudhulumiwa kwa ajili ya imani yao, watu wanapoteza makazi kwa ajili ya imani yao
na tumeshuhudia wakimbizi katika kila kona ya dunia hii na hasa afrika yetu. Mauaji
ya watoto na utoaji mamba na kila aina ya unyanyasaji mbalimbali.
Haya ni matokeo
ya kutokuwa na huruma kwa wengine. Na sisi sote kwa kila mmoja wetu kwa namna
moja ama nyingine tumekuwa wazito wa kutowakimbilia wenye shida na
kutokuwasaidia na haya yote yanatokana na kutojali na kuguswa na matatizo ya wengine
na kuona ni ya watu.
Mfano hivi
karibuni tumesikia maafa yaliyotokea kule Kagera ya tetemeko la ardhi ambalo na
sehemu tofauti mabweni ya wanafunzi kuungua moto, mafuriko na mambo kadha wa
kadha yanayolikumba taifa lakini watu hatujali wala kuguswa kana kwamba
hayatuhusu.
Huko ni kukosa
moyo wa huruma na upendo.
Kwa kusoma alama
za nyakati Ndio maana Baba mtakatifu April 11, 2015 aliitisha mwaka wa Yubilee
ya Huruma ya Mungu ili kuhamasisha kupendana, kushikamana, kujaliana na
kusaidiana na hivyo huruma iongoze maisha yetu na tuweze kuguswa na kusaidia
wahitaji katika taifa letu,” amesema Askofu Kyaruzi.
Kwa zaidi ya
miaka 20 jimboni Sumbawanga kumekuwa kukifanyika kongamano kubwa la mahubiri ya
hadhara maarufu kwa jina la poplamission ambalo hubeba ujumbe wa Mwaka wa
Kanisa uliotangazwa na Baba Mtakatifu ambalo tamasha hili hufanyika kila mwezi
wa tisa kuelekea dominika ya kutukuka kwa msalaba na kuhudhuriwa na maelfu ya
wakristo na wasio wakristo.
Kongamano hilo huhitimishwa
katika vilele vya mlima wa Itwelele
(milanzi) mlima ambao ni maarufu sana kwa historia ya kabila la wafipa ambapo inasadikika ndipo
chimbuko la kabila hili kupitia kwa viongozi wake wa jadi (watemi) ambapo juu
ya kilele chake kuna msalaba wa hija ambapo watu mbalimbali hufika kusali na
kufanya hija na novena zao .
Comments
Post a Comment