Papa amteua Padri Kassala kuwa Askofu mpya Jimbo la Geita
Baba Mtakatifu Fransisko amemteua Padri Flavian Kassala kuwa askofu mpya wa Jimbo Katoliki Geita. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Raymond Saba kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla anayo furaha kutangaza kuwa Papa Fransisko amemteua Padri Kassala kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Geita. Mpaka wakati wa uteuzi wake Askofu mteule Kassala alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris Mtwara. Askofu mteule Kassala amezaliwa Desemba 4, 1967 katika Parokia ya Sumve, Jimbo Kuu Katoliki Mwanza. Alipata masomo yake ya Sekondari katika Seminari ndogo ya Mtakatifu Pio wa X, iliyoko Makoko, Jimbo Katoliki la Musoma. Alijiendeleza zaidi kwenye Seminari Ndogo ya Sanu Jimbo Katoliki Mbulu. Masomo ya falsafa aliyapata kutoka Seminari ya Mtakatifu Anthony wa Padua- Ntungamo, iliyoko Jimbo Katoliki la Bukoba. Askofu mteule Kassala alijipatia elimu ya Teoloji...