Umoja wa Wamama Wakuu TZ wajenga ofisi mpya Tegeta
UMOJA wa Wamama Wakuu Tanzania (TCAS) umejenga ofisi mpya Tegeta jijini
Dar es Salaam na kufunguliwa rasmi Novemba 9 mwaka huu na Askofu Mkuu wa Jimbo
Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akifungua jengo hilo, Kardinali Pengo amewapongeza watawa
kwa hatua hiyo huku akiwatakia heri kwa kazi ambayo Mungu ameianzisha na
aifikishe kulingana na baraka
alizozitoa.
“Mipango ya Mwenyezi Mungu
kamwe haishindwi, kwa sababu ni yeye anayebariki kila lililo jema. Jambo
la msingi ni kuhakikisha mnaimarisha umoja wenu kwakuwa ninyi ni wamoja,”
amesema Kardinali Pengo.
Aidha mewasisitiza kuwa na ukaribu na Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam .
Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa Umoja wa
Wamama Wakuu Tanzania Sista Gaspara Kashamba ambaye ametoka Shirika la Masista
wa Usambara Jimbo Katoliki Tanga amewashukuru
Maaskofu wote kwa kuwachangia na kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo,
Wamama Wakuu kwa juhudi za kujinyima na kujali umoja wao kwa kutoa michango
bila kuwasahau wakandarasi waliojenga ofisi hiyo.
Amesema nyumba mpya itatumika kama ofisi ya (TCAS), na
malengo yao kwa sasa ni kuhakikisha wanajenga ukumbi na hosteli ya kulala watu.
Kwa upande wake Katibu wa umoja huo Sista Claudia
Mashambo, amemshukuru Mungu kwa kuwapatia ofisi, jambo litakalopanua wigo wa
utumishi wao, kwa kufanya kazi za utumishi kwa ufanisi mkubwa, huku wakiendelea
na mipango ya kujenga hosteli na ukumbi.
Comments
Post a Comment