SHERIA MPYA YA NDOA: PAPA AWATAKA MAKUHANI KUWA KARIBU ZAIDI NA WANANDOA


Ninayo furaha ya kukutana nanyi wakati wa kuhitimisha kwenu mafunzo kwa wahudumu wa Kanisa na walei, mkutano ulioandaliwa na Mahakama Kuu ya Vatican, ukiwa na kauli mbiu Mchakato mpya wa ndoa na hatua zake kwa ngazi zake za juu ni Mafunzo yaliyofanyika Roma, kama pia mafunzo yanayofanyika katika majimbo mengine.  Mafunzo haya ni ya kupewa sifa na kutiwa moyo ili yaweze kutoa mchango na fursa ya utambuzi katika kubadilishana uzoefu kwa ngazi mbalimbali za Kanisa na umuhimu wa hatua za michakato ya sheria.
Ni utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Fransisko Jumamosi 25 Novemba 2017 alipokutana na washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mahakama kuu ya Vatican. Baba Mtakatifu katika  hotuba yake anasema, ni muhimu  kutazama kwa makini Hati mbili za hivi karibuni  zinazohusu “Yesu Kristo Hakimu mwenye huruma” ijulikanayo kama “Mitis Iudex Dominus Iesus” na ile ya “Huruma katika hukumu” maana yake, “Mitis et Misericors Iesus” iliyochapishwa  tarehe 15 Agosti 2015,  na ili hatimaye ziweze kutumika katika michakato  mipya thabiti ya sheria. Hati hizi mbili zimetokana na mantiki ya Sinodi ya mababa na  kielelezo cha mtindo wa Sinodi katika  sehemu nyeti ya safari ya mababa wa Sinodi.
Kwa upande wa masuala yanayohusu utume wa uinjilishaji na wokovu wa roho, ni muhimu Kanisa kurudia kwa upya kutazama  hatua za sinodi ya kwanza iliyofanywa na  jumuiya ya Yerusalem, mahali ambapo Petro na mitume wengine na wanajumuiya nzima chini ya kazi ya Roho Mtakatifu walijaribu kutenda kwa mujibu wa amri ya Bwana Yesu. Hata hivyo Baba Mtakatifu akikumbusha juu ya Sinodi ya familia anasema: hicho ndicho kitendo kilichofanyika katika Sinodi kuhusu familia mahalia ambapo Roho wa umoja na undugu aliongoza wawakilishi Maaskofu kutoka pande zote za dunia kuungana pamoja na kusikiliza sauti ya jumuiya, kujadiliana, kutafakari ili kutafuta mang’amuzi.
Malengo ya Sinodi ya Familia yalikuwa ni kuhamasisha, kutetea familia na ndoa ya kikristo  kwa ajili ya wema wa wanandoa katika maadhimisho ya muungano wao na Kristo. Hata hivyo walikuwa pia watafakari kwa kina na wajifunze hali halisi na maendeleo ya familia katika ulimwengu wa sasa, na zaidi kuhusu  maandalizi ya ndoa, namna ya kuwasaidia wanaoteseka kutokana na kutenguka kwa ndoa zao, mafunzo kwa watoto na mantiki nyingine nyingi.
Kutokana na hayo, Baba Mtakatifu anawapa ushauri warudipo katika jumuiya zao, kwamba wajikite kuwa wamisionari na mashuhuda wa roho ya Sinodi ambayo ni asili, pia wawe kitulizo cha kichungaji, ambayo ndiyo kwanza sheria mpya ya wanandoa, kwa kushirikishana imani na watu wa Mungu  na kwa njia ya upendo. Aidha anasema kuwa, Roho ya sinodi  na kitulizo cha kichungaji viwe ndiyo mtindo wao katika shughuli za uchungaji za Kanisa, hasa katika hatua nyeti ya familia na kutafuta ukweli juu ya wanandoa. 
Na kwa mtindo huo kila mmoja wao, awe mkweli kushirikiana na Askofu ambaye kwanza katika  sheria hizi  mpya zinamtambua nafasi yake thabiti na zaidi katika uamuzi wa michakato iliyo mifupi, kwa maana hiyo Askofu ndiye hakimu wa kwanza wa Kanisa mahalia. Pamoja na hayo katika huduma yao wao wanaitwa kuwa karibu na wale wapweke na mateso ya waamini ambao wanasubiri msaada wa Kanisa ili wapate amani katika dhamiri na utashi wa Mungu juu ya kupokea Ekaristi. Baba Mtakatifu anaongeza; na hapa ndiyo ulazima na thamani ya semina waliyohudhuria. Kwa maana hiyo anawatakia matashi mema  baada ya semina hiyo ili pia  ziweze kuandaliwa hata nyingine zaidi kwa ajili ya kusaidia kuwa na utambuzi wa kina juu ya masuala na mafunzo ya mchakato huu mpya wa sheria ya ndoa. Mafunzo ya ndoa kwa upande wa Kanisa yana uwezo wa kupokea na kuwatuliza  ambao wamajeruhiwa kwa namna nyingi katika maisha, wakati huo huo wawajibike  kulinda muungano mtakatifu wa ndoa.
Halikadhalika ili kuweza kufanya sheria mpya ya mchakato wa ndoa baada ya miaka 2 tangu kutangazwa kwake sambamba na lengo la wokovu na imani kwa waamini wengi waliojeruhiwa katika ndoa zao; Baba Mtakatifu kama Askofu wa Roma na Kharifa wa Mtume Petro ameamua kuweka mantiki msingi katika Hati mbili kwa namna ya pekee  ya Askofu wa Jimbo kama hakimu wa kwanza na pekee katika mchakato mfupi.
Kutokana na kwamba kila Jimbo palipo na Askofu tayari ile ni mahakama na Askofu anakuwa ni hakimu Mkuu kwa mujibu wa Baba Mtakatifu, anasema Askofu ni  (Iudex unum et idem cum Vicario iudiciali); Lakini kutokana na kanuni hii kutafasiriwa kwa namna  ya kuondoa zoezi binafsi la Askofu wa Jimbo, kutuma wawakilishi karibu  kila mahakama, Yeye binafsi anatoa misingi ya maelekezo kuhusiana na wajibu wa  Askofu kwa nguvu ya ofisi yake  kichungaji  na kuthibitisha kuwa ni hakimu mkuu katika mchakato wa muda mfupi wa kijimbo.
Hata hivyo ametoa uwazi ya kwamba kila mchakato jimboni utafanyika bila kuomba ruhusa kutoka katika  taasisi nyingine au katika Makao ya Ubalozi wa Kitume wa Vatican. Amewatakia kila jema katika mafunzo kwa ajili ya wema wa Kanisa na kila mmoja na Bwana awabariki.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican


Comments

  1. je naweza kufuga ndoa na mke akaendelea na dini yake?

    ReplyDelete
  2. Nimefunga ndoa ya kanisa katoliki na Nina watoto wawili. Nikapata nafasi ya kwenda masomoni
    Pamoja na kuhudhuria likizo zangu zote kwa mke wangu. Aliweza kunisaliti na akawa anaishi na mme mwingine nikiwa ktk mwaka wangu wa mwisho wa kumaliza masomo Mara nikapewa hati ya malalamiko kutoka mahakamani kuwa nimemtelekeza miaka mitatu, hakika nilipagawa anadai talaka, Je, kanisa katoliki linaweza niruhusu kufunga ndoa nyingine na kwa kuwa mwenza wangu anaishi na mtu mwingine? Kwa vile mke tayar anaishi na mme mwingine. Ni mini mstakabali wangu na hatima yangu?

    ReplyDelete
  3. mapundacaspary123@gmail.com
    Nimefunga ndoa ya kanisa katoliki na Nina watoto wawili. Nikapata nafasi ya kwenda masomoni
    Pamoja na kuhudhuria likizo zangu zote kwa mke wangu. Aliweza kunisaliti na akawa anaishi na mme mwingine nikiwa ktk mwaka wangu wa mwisho wa kumaliza masomo Mara nikapewa hati ya malalamiko kutoka mahakamani kuwa nimemtelekeza miaka mitatu, hakika nilipagawa anadai talaka, Je, kanisa katoliki linaweza niruhusu kufunga ndoa nyingine na kwa kuwa mwenza wangu anaishi na mtu mwingine? Kwa vile mke tayar anaishi na mme mwingine. Ni mini mstakabali wangu na hatima yangu?

    ReplyDelete
  4. Je , ninaweza kumuoa Binti ambaye mamangu ndo kamsimamia kwenye ubatizo?

    ReplyDelete
  5. Nilioa mwanamke wa kiisilam baadaye alibadli dini na kurudi kwenye dini yake na ameolewa ndoa ya kiisilamu. Je, Mimi MKATOLIKI nitafanyaje naruhusiwa kuoa mke mwingine?

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI