MAKARDINALI, MAASKOFU WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI WAOMBEWA NA PAPA FRANSISKO

Hapo jana (Ijumaa tarehe 3 Novemba), Baba Mtakatifu Fransisko ameadhimisha misa Takatifu kwa ajili ya kuwaombea marehemu wote makardinali na Maaskofu waliokufa kwa kipindi cha mwaka huu. Katika mahubiri yake anasema, kwa mara nyingine tena Liturujia ya siku inatuweka katika hali halisi ya kifo na kukumbusha watu tulioshi nao karibu pia wale walio tutendea mema. Lakini vile vile Liturujia inaongeza matumaini yetu kwa ajili yao na hata sisi wenyewe.
Somo la kwanza linaeleza juu ya matumaini ya kufufuka kwa wale wenye haki.Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. (Dn 12,2). Baba Mtakatifu anaongeza, kifo ndiyo upeo wa mwisho kuondokana na makona kona ambayo yako mbele yetu katika ulimwengu huu: Njia ya maisha inayotupeleka katika mungano na Mungu au njia ya kifo inayotupeleka mbali na Yeye. Wangi  ambao watafufuka katika maisha ya milele, wako wanasubiri kama wale ambao Kristo amemwaga damu yake kwa ajili yao. Hawa ni undi kubwa kwa neema ya huruma ya Mungu ambayo inajieleza katika hali halisi ya maisha ambayo yana ushindi juu ya kifo kwakuwa kuna ufufuko.
Injili inaimarisha matumaini yetu: “ Mimi ni mkate wa uzima ushukao mbinguni, kila aulaye mkate huo ataishi milele (Yh 6,51). Hayo ni maneno yanayoeleza sadaka ya Kristo Msalabani. Yeye alikubali kifo kwa ajili ya kuwakomboa watu ambao Baba yake alimkabidhi, ni watu ambao walikuwa wamekufa katika utumwa wa dhambi. Yesu amekuwa kaka yetu na kushiriki  maisha yetu hadi kifo. Ni kwa njia ya upendo wake , alivunja minyororo ya kifo na kutufungulia mlango wa maisha. Kwa kulishwa mwili wake na damu yake sisi sote tunaungana na upendo wake mwaminifu, ambao unatupatia matumaini ya ushindi hadi mwisho dhidi ya ubaya, mateso na kifo.
Kwa nguvu za agano la Mungu kwa upendo wa Kristo sisi sote tunatambua kuwa umoja kwa walio kufa syo wa kufikirika, bali ni utashi, ni jambo halisi. Imani tunayokiri katika ufufuko inatupelekea kuwa watu wa matumaini, Baba Matakatifu anasisitiza, na wala siyo kuhangaika, sisi ni watu wa maisha na siyo wa kifo , kwasababu Yeye anatufariji na kutoa ahadi za maisha ya milele yanayotokana na umoja na Kristo Mfufuka.
Imani hii inayowaka ndani mwetu kwa njia ya Neno la Mungu inatusiadia kuwa na tabia ya matumaini mbele ya kifo. Hiyo ni kutokana na kwamba Yesu mwenyewe alituonesha kuwa kifo hakina neno la mwisho bali ni upendo wa huruma ya Baba yake ambaye anajionesha kwetu na kutufanya tuishi katika muungano naye daima.
Tabia msingi ya maisha ya kikristo ni matarajio ya mwisho ya kukutana na Mungu, kama zaburi  ( 42,3) isemavyo : Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai, lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Baba Mtakatifu anaongeza kusema, hayo ni maneno yanaojieleza kwa namna ya kutoa mshangao wa matarajio, kwa maana ya kuona kiu ya upendo, ya uzuri na hata ya furaha na matumaini kwa Mungu.
Maneno ya mzaburi yaliyojiweka kama muhuri katika mioyo ya makardinali na maaskofu ambao leo hii wanakumbukwa: wao wameondoka baada ya kuhudumia Kanisa na watu wa Mungu walio kabidhiwa , na katika mtazamo wa umilele. Baba Mtakatifu anasema, tukiwa tunashukuru Mungu kwa huduma yao na ukaribu walioonesha katika Injili na Kanisa, ni vema kurudia na mtume Paulo kuwa matumaini hayakatishi tamaa, na kwa maombezi ya Maria maa Yetu Mtakatifu atusaidie ili tuweze kushiriki katika meza ya Bwana , ambayo kwa imani na upendo tumeonja kipindi chote cha hija ya hapa duniani.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI