Askofu Mkuu Rugambwa awa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu
BABA Mtakatifu Fransisko amemteua Askofu
Mkuu Protase Rugambwa kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa
Watu. Askofu Mkuu Rugambwa alizaliwa tarehe 31 Mei 1960 huko Bunena-Bukoba
nchini Tanzania, akapata Daraja ya Upadri kutoka kwa Papa Yohane Paulo II
alipotembelea Tanzania tarehe 2 Septemba 1990 na kuwa padri wa Jimbo Katoliki
Rulenge-Ngara.
Tarehe
18 Januari 2008 aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, na Juni 2012
aliteuliwa kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na
Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari.
Aidha
Baba Mtakatifu amemteua Monsinyo Giovanni Pietro Dal Toso kuwa Katibu Mwambata
wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu.
Comments
Post a Comment