SIKU YA MASIKINI DUNIANI: PAPA FRANSISKO ATOA RAI
Tunayo furaha kubwa ya kuumega mkate wa Neno na baadaye utamegwa na kuupokea mkate wa Ekaristi, kirutubisho cha safari ya maisha. Na ni furaha kwa wote kwani hakuna asiye hitaji maana wote ni waombaji wa jambo muhimu la upendo wa Mungu anayetoa maana ya maisha, yaani maisha yasiyo na mwisho,na kwa njia hata sisi leo hii tunaamsha mikono yetu kupokea zawadi kutoka kwake.
Ni sehemu ya mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo siku ya Jumapili 19 Novemba, asubuhi wakati wa Kuadhimisha Siku ya Masikini Duniani 2017 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Mjini vatican. Baba Mtakatifu akiendelea kufafanua juu Injili ya siku ya Jumapili anasema, Injili inaelezea zawadi hizo, kwa maana sisi tumepewa talanta za Mungu kwa mujibu wa uwezo wa kila mmoja alio nao (Mt 25,15). Ni lazima kuwa na utambuzi wa talanta hizo tulizo nazo machoni pa Mungu. Hakuna mtu yoyote ambaye anaweza kufikiria kuwa hana faida au kuwa maskini kiasi cha kutoweza kutoa chochote kwa wengine. Sisi tumechaguliwa na kubarikiwa na Mungu ambaye anashahuku ya kututuliza kwa zawadi zake, kama vile baba na mama wanavyo tamani kuwapa watoto wao. Mbele ya Mcho ya Mungu asiye bagua yoyote anamkabidhi kila kila mmoja utume wake.
Hayo inajidhihirisha kwamba, ni baba wa pendo lakini ambaye anatuwajibisha, kwa maana ya kutazama Injili ikieleza juu ya watumwa waliopewa talanta ziweze kuzaa mara dufu. Lakini inaonekana wakati wale wawili wa kwanza, waliweza kutimiliza utume waliopewa, mtumishi wa tatu hakuweza kuzalisha talanta mara dufu badala yake akamrudishia jinsi ilivyo Bwana wake, na kusema, aliogopa akaenda kuifukia chini ya ardhi hiyo talanta na hivyo aipokee iliyo yake jinsi ilivyo (Mt 25).
Baba Mtakatifu Francisko anaongeza kusema, lakini mtumwa huyo alipokea maneno makali mno yasemayo kwamba,“wewe mtumwa mbaya na mlegevu”. Je ni kitu gani hakupenda huyo Bwana kwake? Akifafanua anasema, ni neno moja ambalo kwa sasa tunaliita “kutotimiza wajibu”. Akifafanua, zaidi anasema, ubaya wake ulikuwa ule wa kutofanya mema. Lakini hata hivyo hata sisi mara nyingi tunayo mawazo ya kwamba hatujafanya ubaya na hivyo tunajifurahisha na kuendelea kuishi jinsi tulivyo kana kwamba sisi ni wema na wenye haki.
Lakini kwa kufikiria hivyo, Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, ipo hatari ya kufananishwa na mtumwa mbaya: kwa maana hata yeye hakufanya jambo baya, kutokana na kwamba hakuharibu hiyo talanta, badala yake alikwenda akahifadhi chini ya ardhi. Yeye hakufanya chochote cha ubaya basi. Mungu siyo mkaguzi wa kwenda kutafuta tiketi ambazo bado hazijatiwa muhuri, ni Baba wa kutafuta watoto wake ambao aliwapatia zawadi na mipango yake .
Ni huzuni anaongeza, iwapo Baba wa upendo hapokei jibu la upendo wa ukarimu kutoka kwa watoto wake, ambao wana vizingiti katika kuheshimu sheria, kutimiza amri, lakini baadaye wana kukumbuka kuwa kuna wafanyakazi wengi wanaopata mshahara kwa baba na wanakula na kusaza (Lk 15,17).
Mtumwa mbaya pamoja na kupokea talanta ya Bwana anayependa ishirikishwe na kuzaa matunda mara mbili alikwenda kaitunza kwa wivu wake, kwa maana alifurahia kufanya hivyo. Hiyo ni kuthibitisha kuwa mtu wa kufanya hivyo siyo mwaminifu kwa Mungu maana anangaikia kuhifadhi, kuhifadhi tunu za kale. Injili inaeleza kuwa yule mwenye talanta mpya ni mwaminifu kweli kwa maana anayo mantiki sawa na Mungu, siyo tu kukaa bila kuwajibika. Ni mtu ambaye anajikitia kwa dhati kwa ajili ya upendo wa maisha ya wengin na haiwezekani kuicha jinsi ilivyo kwa ajili yake na ndiyo jambo muhimu la kutimiza hasa wajibu.
Kutotimiza wajibu ni dhambi kubwa mbele ya maskini Baba Mtakatifu amesema. Hiyo inatoa jina kamili la utofauti kwa maana wapo wengine wanaosema inanihusu nini;siyo shauri langu bali ni kosa la jamii. Wanageuka pembeni wakati ndugu wanayo mahitaji, ni kubadilisha mkondo inapoonekana suala fulani ni nyeti, linakera, au kuwa na hasira mbele ya mabaya japokuwa si ya kweli.
Lakini Mungu hataomba kama tulikuwa na haki au hasira, yeye atauliza iwapo umetenda mema. Katika mahubiri Baba Mtakatifu anaendelea kufafanua jinsi gani ya kumfurahisha Mungu, akitoa mfano rahisi ya kwamba unapotaka kumzawadia rafiki yako mpendwa, kwanza lazima ujue kitu gani anapendelea ili kuhepuka zawadi siyo stahili kwa rafiki yako na ndivyo hivyo unapotaka kutoa zawadi kwa Bwana ni lazima kuzipata kwa njia ya Injili yake. Na katika Injili ya Matayo (Mt 25,40), inasema “kile ambacho mlitoa kwa yule mdogo, mmefanya kwa ajili yangu” .
Ndugu wapendwa wa Mungu ni wale wenye njaa, wagonjwa,wageni,wafungwa, walioachwa pweke wanaoteseka bila kuwa na paa la nyumba na wote walio baguliwa. Katika sura yao tunaweza kufikiria kuwa ni sura ya Mungu, katika midomo yao, hata kama imefungwa na uchungu wao, katika maneno yake anasema ni mwili wake.(Mt 26,26). Kwa maskini Yesu anabisha mlango wa moyo wake kwa maana anayo kiu na anataka upendo. Tukishinda utofauti kwa jina la Yesu na kuwatumikia walio wadogo, basi sisi ni marafiki wema na waamini kwa maana ndiyo wajibu huo. Baba Mtakatifu akielezea juu ya somo la kwanza kuhusu mwanamke: Mungu anafurahia kuona tabia ya mfano wa mwanamke katika somo la kwanza ambaye ni mwenye nguvu, anafungua mikono yake kwa ajili ya masikini na wahitaji (Meth 31,10.20).
Leo hii tunaweza kujiuliza ni kitu gani kinahitajika katika maisha yangu? Katika utajiri unaopita ambapo dunia haishibishwi nao , au katika utajiri wa Mungu anayetoa maisha ya milele? Uchaguzi huo uko mbele yetu kuchagua kuishi ili upate ardhi hii au kutazama juu mbinguni. Kwani ili uweza kuingia katika ufalme mbingu hauitaji kile ulicho nacho,bali kile unachotoa kwa wengine!
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Comments
Post a Comment