KITABU CHA HISTORIA YA MAWASILIANO YA BABA MTAKATIFU CHAZINDULIWA: UTARATIBU WA MAWASILIANO WAFAFANULIWA


Tabia ya Baba Mtakatifu katika mawasiliano daima ni nyepesi, mtazamo na ishara zake ndiyo mtindo wake. Ni maneno ya Monsinyo Dario Vigano’ Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican wakati wa kuwasilisha Toleo Jipya la Kitabu kinacho eleza historia mawasiliano ya  Papa Francisko, chenye kichwa cha habari ” Mawasiliano ya Papa katika nyakati za kuunganishwa na mawasiliano duniani (toleo jipya 2017) katika Makao ya Kituo cha Habari Italina (RAI) Mjini Roma.
Katika maelezo ya Monsinyo Vigano' juu ya kitabu hicho anasema, kinajikita zaidi kufafanua mchakato mzima wa mawasiliano ya Baba Mtakatifu, kwa njia hiyo kitabu kinaunda hata uhusiano wa watu wanaotazama moja kwa moja au wanaotazama kwa njia ya mitandao.
Mawasiliano ya Baba Mtakatifu ni ya moja kwa moja, pamoja na kuwa tofauti au mbali na uteknolojia. Yeye anao uwezo wa kuwasilisha ujumbe wa haraka na kawaida! Kwa njia hiyo anasema wakati mwingine ni changamoto iliyopo kwa kazi ya mitandao ya Vatican ya kwa na  ule ya utayari kutambua kwa haraka kile ambacho kimesahulika katika protokali.
Hata hivyo akisifia  waandishi wa kitabu anasema kuwa,wameonesha ni jinsi gani, Baba Mtakatifu pia anajibu  kwa vyombo vya habari vinapotoa habari zisizo za kweli kuhusu yeye, na kwamba ni fursa ya kuchangamotisha na kutoa hoja . Na mwisho waandishi wa habari wameuliza swali kuhusu simu ambazo Baba Mtakatifu amegusia wakati wa maadhimisho ya ibada Takatifu. Monsinyo Vigano' anaunga mkono juu ya kuwa makini na simu kwa maana ni lazima kutambua jambo Takatifu la Ekaristi wakati huo, kuliko kutawaliwa na jambo la kusumbua " ndani ya mfuko" na "nje ya mfuko".Kwa maana hiyo ni kupokea na kujikita jambo la muhimu wakati wa maadhimisho ya misa Takatifu!.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI