MAPADRI WENYE TAMAA WAONYWA
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka amewaasa mapadri kukaa chonjo na mali za ulimwengu huu unaopita ili wasiingie matatani na kuipoteza imani yao safi. Rai hiyo ameitoa hivi karibuni katika adhimisho la Misa Takatifu na kutoa Sakramenti ya Daraja Takatifu ya Upadri kwa Shemasi Peter Fabian Kulwa hivi karibuni. Akitoa mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi Kipalapala Tabora, Askofu Mkuu Ruzoka amewataka mapadri kupeleka upendo wa Kristo kwa watu wote bila ya ubaguzi wowote. Amesema Mtakatifu Matayo mtume na mwinjili alikubali kuacha kazi yake nzuri ya mshahara akakubali kumfuata Kristo, vivyo hivyo na padri anapoitwa hana budi kuacha yale yote yasiyoendana na wito mtakatifu wa upadri na kumsikiliza Kristo anachomtaka akifanye kwa watu wake. Pia Askofu Mkuu Ruzoka amesema wito wa upadri ni zawadi toka kwa Baba Mungu ambayo padri anazawadiwa bila mastahili yake mwenyewe. Na kama mtu atasema nataka kuwa padri bila kuitwa n...